HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA KITENGO CHA USTAWI WA JAMII
i. Familia na Watoto
Katika kitengo hiki huduma zinazotolewa ni
•Usuluhishi wa ndoa zenye mafarakano:
• Huduma za matunzo kwa watoto walio katika ndoa zenye mfarakano.
•Huduma ya matunzo kwa watoto waliozaliwa nje ya ndoa.
•Malezi ya Kambo na kuasili.
•Huduma ya Makao ya kulelea watoto yatima na Walio katika mazingira hatarishi.
•Huduma ya Malezi, Makuzi na maendeleo ya Watoto ya awali ya watoto Wadogo.
•Huduma ya malezi, matunzo na ulinzi shirikishi jamii kwa watoto. Timu ya Ulinzi na Usalama ya Mtoto ya wilaya imeundwa na timu nyingine 5 katika ngazi ya kata zimeundwa.
ii. Huduma kwa wazee na watu wenye ulemavu
Kitengo hiki kinatoa huduma kwa kuzingatia sera,miongozo, kanuni na sheria. Lengo kuu ni
•kuwapa taarifa na ushauri juu ya upatikanaji wa ajira.
•Kuwaunganisha na taasisi za fedha kwa ajili ya kupata mitaji ya biashara ndogo ndogo
•Kutoa ushauri wa kitaalamu ili kuweza kumudu shughuli wanazozifanya
•Kuwezesha kuanzisha vyama/mabaraza ya wazee.
•Kuunganisha wazee na makazi ya wazee ili kupata matunzo.
iii.Marekebisho ya Tabia na Haki ya mtoto kisheria
•Huduma za kusimamia haki za watoto.
•Huduma katika Mahabusi za watoto..
•Huduma kwa watoto watukutu.
•Huduma zitolewazo kwa watoto waliofanyiwa ukatili na kufanya utetezi mahakamani.
Huduma zote hizi ni bure unachotakiwa ni kufika ofisi ya Ustawi wa jamii Wilaya kwa maelekezo zaidi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.