Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mashaka Gambo amewataka watumishi wa Halmashauri ya Arusha kufanya kazi kwa kushirikiana kama timu na zaidi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Mkuu wa mkoa Gambo amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Makao Makuu ya halmashauri ya Arusha wilaya ya Arumeru kwenye Ukumbi wa Mikutano siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano iliyoanza leo katika halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru.
Amesisitiza kuwa kila mtumishi anafahamu majukumu ya kazi yake, wajibu wake pamoja na mipaka ya kazi yake hivyo ni vema kila mtu akaheshimu majukumu ya kila mtumishi na kufanyakazi kwa pamoja kama timu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.