Na. Elinipa Lupembe.
YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU.
##Halmashauri iweke mikakati ya kudumu ya ukusanyaji wa mapato kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi pamoja na kukiwezesha kitengo cha mapato na biashara, kutekeleza majukumu yake, ili kufikia malengo ya ukusanyaji mapato yaliyowekwa kwenye bajeti.
##Mawakala wa ukusanyaji mapato waliowe fedha zao kwa wakati mara tu baada ya kuziwasilisha ili kuepuka madeni na kubiresha utendajikazi.
##Halmashauri izingatie utaratibu wa kutumia asilimia 40% ya mapato ya ndani, kutekeleza miradi ya maendeleo.
##Kitengo cha TASAF kuwasilisha maoni ya wajumbe wa Baraza Serikali kuu, juu ya marekebisho ya uwajibikaji wa Kamati za Usimamizi miradi ya TASAF ngazi ya jamii- CMC ili kutoa nafasi kwa Madiwani kuzihoji kamati hizo kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa miradi hiyo.
##Idara ya Mazingira irndelee kutoa elimu ya utunzaji mazingira kwa wananchi wanaoishi kuzunguka mlima Kivesi, ulioko kata ya Kiutu,pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria, wale ambao wanaoharibu mazingira, kutokana na wananchi hao kuvamia hifadhi ya mlima huo kwa kukata miti, kulisha mifugo jambo ambali linasababisha ukame na mmomonyoko wa udongo.
##Vikao vya Kamati za kudumu vya kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo, vifanyike kwa wakati ili kutoa fursa ya kufanya kujipima na kufanya tathmini ya utekelezaji wa maazimio kwa wakati.
## Halmashauri ienfee kuikumbusha Serikali Kuu kulipa deni la Fidia ya Shamba la Lakilaki, fedha ambazo halmashauri inadai kwa muda mrefu sasa.
##Wameishukuru serikali ya awamu ya tano,inayoongozwa na Rais wa wanyonge, Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuwezesha halmashauri ya Arusha, kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwenye sekta ya Elimu, Afya, Maji na miundombinu ya umeme, miradi iliyowezesha wananchi kupata huduma bora kwa kasi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, mhe. Baraka Simon akihitimisha maazimio ya mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya tatu, mwaka wa fedha 2019/2020.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani, halmashauri ya Arusha wakifuatilia mijadala wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya tatu, mwaka wa fedha 2019/2020.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani, halmashauri ya Arusha wakifuatilia mijadala wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya tatu, mwaka wa fedha 2019/2020.
Diwani wa Viti Maalum, Mhe. Yasimi Bachu akichangia hoja wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya tatu, mwaka wa fedha 2019/2020.
Diwani wa kata ya Ilkiding'a, Mhe. Loth Mungaya, akichangia hoja wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya tatu, mwaka wa fedha 2019/2020.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.