Na. Elinipa Lupembe.
# Afisa Elimu Sekondari kuandaa majina ya wanafunzi 49 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 na mpaka sasa hawakuripoti shuleni, majina hayo yakiainisha kata na maeneo wanayotokea ili madiwani kushiriki kutafuta ukweli wa mahali walipo wanafunzi hao.
# Wamejadili kuangalia namna ya kutungwa kwa sheria ndogo ya halmashauri itakayowezesha ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara ya kupangisha nyumba, kwa kuwa nyumba zinapangishwa kwa bei kubwa na hakuna kodi wanayokatwa wafanyabiashara hao.
# Wakala wa barabara mijini na vijijini - TARURA kuandaa utaratibu wa kuweka alama kwenye hifadhi za barabara kwenye maeneo ambayo tayari wananchi wameacha kwa ajili ya hifadhi za barabara ili kusiwepo na uvamizi mwingine katika maeneo hayo.
# Zaidi TARURA kuanza utaratibu wa kuweka vibao pia, kwenye barabara ambazo bado hazijavamiwa na wananchi ili kuzuia uvamizi, kwa kuwa uvamizi huo, husababishia wananchi hasara kubwa pindi wanapobomolewa nyumba zao.
# Maafisa Watendaji wa kata na Vijiji waainishe maeneo ya hifadhi za barabara zote katika maeneo yao kwa kuzingatia vigezo vya barabara hizo kisheria, kwa lengo la kuzuia ujenzi wa uvamizi wa barabara pamoja na ubomoaji wa nyumba zitakazoje gwa kwenye hifadhi za barabara.
# Kuainisha minara yote ya simu iliyoko ndani ya halmashauri ya Arusha ili kuona kodi za kila mnara zinalipwa wapi.
# Idara ya Maji kushughulikia miradi midogo ya maji, ikiwemo miradi Mindeu, Ilkiushini, OLOMULO ili kuondoa changamoto zinazosababisha miradi hiyo kutokutoa maji na kusababisha kero kubwa kwa wananchi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.