Na. Elinipa Lupembe.
## Waheshimiwa Madiwani wanatakiwa kushirikiana na watalamu pamoja na wadau wa maendeleo wa halmashauri ili kuweka mkakati wa kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao, kwa kuwa madiwani wamebeaba taswira halisi ya changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.
## Waheshimiwa Madiwani wana jukumu la kuhamasisha wananchi na wadau wa maendeleo katika maeneo yao, kushiriki katika ujenzi wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na nyumba za walimu, ili kupunguza changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa unaotokana na elimu bila malipo, pamoja na kuwezesha walimu kuishi karibu na shule wanazofundisha..#Menejimenti imeagizwa kuendelea kuikumbusha serikali kupitia Tume ya Utumishi kupata wahtumishi katika sekta ya afya, sekta amabyo inaupungufu mkubwa wa watumishi hao, halmashauri inatakiwa kuwa na jumla ya watumishi 775 lakini mpaka ssasa ina watumishi kati ya 286, jambo ambalo linawapa mzigo mkubwa watumishi hao pamoja na kudhorotesha utoaji wa huduma za afya kwa wanachi.
## Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia REA kupitia upya utaratibu wa mtandao wa usambazaji wa umeme katika vijiji vya halmashauri ya Arusha, kwa kuwa mpaka sasa vijiji vingi havijapata umeme ukilinganisha na idadi ya vijiji 67 vya halmashauri hiyo, hata hivyo katika vijiji vichachw vilivyopata umeme ni wananchi wachache sana waliopata huduma hiyo ya Umeme.
## Wakala wa Barabara mijini na vijijini (TARURA) halmashauri ya Arusha, imetakiwa kuendelea kufanya matengenezo katika barabara za ndani ya halmashauri, kwa kuwa miundo mbinu ya barabara nyingi ni mibovu na kusababisha kero kwa wananchi.
## Wananchi wa halmashauri ya Arusha, wamesisitizwa kwenda kupata chanjo dhidi ya UVIKO 19, chanjo inayotolewa bure na serikali katika vituo vya afya vilivyoainishwa, msisitizo mkubwa ukiwa kwenye makundi maalum yaliyo kwenye hatari kubwa, ikiwemo watu wenye magonjwa sungu, watu wenye umri mkubwa wa kuanzia miaka 50, walimu pamoja na wahudumuw a afya, huku akiwataka Waheshimjwa Madiwani kuwa mfano wa kuchanja na kuwahimisha wananchi wao kuchanja.
## Aidha wananchi wamesisistizwa kuendelea kujihadhari na UVIKO 19 kwa kufuata mael3kezo yanayotolewa na wahudumu wa Afya, ikiwemo kula chakula bora chenye virutubisho vyote ili kuimarisha kinga ya mwili, kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima, kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji tiririka, kutumia vitakasa mikono, pamoja na kuvaa barakoa.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.