Halmashauri ya Arusha inaungana na mataifa yote Duniani kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji inayofanyika kuanzia tarehe 1-7 Agusti yenyeKauli Mbiu ya "Wezesha Wazazi; Kufanikisha Unyonyeshaji"
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera anawakumbusha wazazi umuhimu wa kunyonyesha mtoto mara baada ya kujifungua, umuhimu wa ziwa la mama kwa mtoto, namna bora ya unyonyeshaji pamoja namna ya kukamua na kuhifadhi maziwa kwa mama anayemuacha mtoto kwa muda.
Aidha ameitaka jamii kuwapa fursa wazazi ya kuwanyonyesha watoto, kwa kuwasaidia na kuwahudumia ili kufanikisha njia sahihi za unyonyeshaji, pamoja na kumpa mzazi faragha pindi anapojifungua ili apate muda mrefu wa kumnyonyesha mtoto.
Maziwa ya Mama ni bora kwa mtoto kuliko aina yoyote ya maziwa au mchanganyiko wa vyakula vingine.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.