Haya hapa maelekezo waliyopewa wenyeviti wa vijiji na vitongoji mara baada ya kula kiapo cha kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha miaka mitano:-
- Serikali ya Kijjiji ndio msingi wa Serikali Kuu, msingi ukiandaliwa vizuri, kila kitu kitakwenda vizuri, maendeleo ya taifa hili yanaanzia kijijini hivyo ni jukumu la Mwenyekiti wa Kijiji ni kusimamima vema maendeleo ya vijiji vyao kwa maendeleo ya Taifa.
-Cheo ni dhamana, wananchi wamekuamni, una wajibu na jukumu kubwa la kuwatumikia wananchi na sio kuwa watawala, kwa mabavu na ubaguzi.
- Jiepusheni na vitendo vya rushwa, tatueni kero za wananchi, kwa kuwashirikisha katika utekelelezaji wa shughuli zote za maendeleo kijijini kwenu, simamieni Sheria, kanuni na miongozo ili muweze kutenda haki.
- Serikali inatoa fedha za miradi moja kwa moja kwenye akaunti za vijiji, Mna jukumu kubwa la kusimamia miradi ya maendeleo na kuhakikisha fedha zote zinatumika kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha za Umma.
- Ni wajibu na ni haki ya mwananchi, kufahamu shughuli za maendeleo zinazofanyika kijijini, Ni takwa la kisheria kufanya Mkutano mkuu wa Kijiji kila baada ya miezi mitatu, fanyeni mikutano hiyo na kuwasomea wananchi taarifa ya Mapato na Matumizi.
- Shirikianeni na watalamu wa ngazi ya kijiji na kata kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yenu, simamieni fedha za serikali kwa uaminifu, hakikisheni fedha zote zinazoingia na kutoka ziko kwenye kumbukumbu na wananchi wapewe taarifa hiyo.
- Migogoro ya Ardhi ni changamoto, ni jukumu lenu kutatua changamoto hiyo, epukeni rushwa, tendeni haki, simamieni sheria ili kuhakikisha hakuna mgogoro mwingine unaoibuka katika kipindi cha uongozi wenu.
- Shirikisheni wananchi na wadau ndani ya maeneo yenu, kuibua miradi na kuchangia maendeleo yenu, badala ya kusubiri Serikali au wafadhili kutoka nje ya nchi, simamieni maendeleo yenu yaletwe na nyinyi wenyewe.
-Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa Mheshimiwa Rais John Magufuli, imewekeza nguvu kuwahudumia wananchi hasa wanyonge,ungeni mkono juhudi za Rais, wahudumieni wananchi bila kuwabagua, tatueni kero zao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.