Na. Elinipa Lupembe.
Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu, ametoa taarifa ya vifo vya Watu 2, waliofariki jana kutokana na Ugonjwa wa Corona, wote ni wanaume, mmoja akiwa na umri wa miaka 51 na mwingine miaka 57, wote ni watanzania na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Waziri Ummy amefafanua kuwa vifo hivyo, vimefanya idadi ya vifo kufikia 3, tangu mgonjwa wa kwanza alipothibitika hapa nchini.
Aidha Waziri huyo, ametoa taarifa ya ongezeko la visa vingine vipya vya watu 5, waliogundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya COVID 19, wote wakiwa ni watanzania, na kufikisha jumla ya visa 32 mpaka kufikia jana tarehe 10 Aprili,2020 nakuongeza kuwa kati ya hao, wagonjwa watano wamekwishapona.
Hata hivyo Waziri Ummy, amewasisitiza watanzania, kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona, kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, maelekezo yanayotolewa kwa njia mbalimbali.
****** CHUKUA TAHADHARI, JIKINGE NA CORONA*****
1. NAWA MIKONO YAKO KWA MAJI TIRIRIKA NA SABUNI, PAKA SABUNI SUGUA MIKONO YAKO KWA SEKUNDE 20, KISHA SUUZA KWA MAJI SAFI.
2. ACHA NA EPUKA KUGUSA USO WAKO KWA KUWA VIRUSI VYA CORONA VINAINGIA MWILINI KWAKO KUPITIA MDOMO, PUA NA MACHO KWA KITENDO CHA WEWE MWENYEWE KUVIBEBA KWA MIKONO YAKO HIVYO NAWA MIKONO KILA MARA.
3.EPUKA KUGUSA VITU VISIVYO VYA LAZIMA, VIRUSI VYA CORONA VINAKAA KWENYE VITU TUNAVYOVITUMIA KILA SIKU KWA MASAA KADHAA, VITU KAMA CHUMA, MBAO, SIMU, REMOTE, NGUO HIVYO NAWA MIKONO KILA UNAPOGUSA VITU HIVYO.
4.UNAPOPIGA CHAFYA AU KUKOHOA ZUIA/FUNIKA KINYWA NA PUA KWA KIWIKO CHA MKONO WAKO AU KITAMBAA KUEPUKA KUSAMBAZA VIRUSI VYA CORONA. USIZUIE KIKOHOZI AU CHAFYA KWA KIGANJA CHA MKONO WAKO.
5.TUMIA VITAKASA MIKONO 'SANITIZER' KWA KUPAKA MARA KWA MARA UKIWA KWENYE MIZUNGUKO YAKO YOTE AU ENEO LAKO LA KAZI.
6.EPUKA MISONGAMANO YA AINA YOYOTE, KAA AU SIMAMA UMBALI WA ZAIDI YA MITA MOJA NA MTU MWINGINE.
7.WAZAZI HAKIKISHENI MNAWEKA NDOO ZA MAJI TIRIRIKA NA SABUNI KWENYE MALANGO YA MABOMA YENU, NA KUWAHIMIZA WATOTO KUNAWA MIKONO KILA MARA, HUKU MKIHAKIKISHA WAGENI WANAOINGIA KWENYE NYUMBA ZENU WANANAWA MIKONO KABLA YA KUINGIA NDANI NA PINDI WANAPOTOKA.
8.EPUKA SAFARI ZISIZO ZA LAZIMA, NI VEMA KUTULIA NYUMBANI KAMA HUNA SHUGHULI ZA MSINGI ZA KUFANYA KWENYE MAENEO YENYE MISONAGAMANO.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.