Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jafo, ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, miradi ambayo inafanyika kwa kiwango cha kuridhisha hasa kwa kuzingatia vigezo vya thamani ya pesa na kukamilika kwa wakati.
Waziri Jafo, ameweka wazi hisia zake, alipotemblea na kukagua mradi wa ujenzi na upanuzi wa Kituo cha Afya cha Mbuyuni, kata ya Oljoro na kujionea namna kituo hivyo kilivyojengwa kwa utalamu mkubwa, huku kikiwa tayari kimeanza kufanyakazi ya kuwahudumia wananchi wa kata ya Oljoro na Kata za jirani za mkoa wa Manyara.
Waziri Jafo licha ya kuwapongeza watendaji, kwa kuongozwa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muri pamoja na watendaji wa halmashauri ya Arusha, amekiri kujivunia sana utekelezaji wa miradi, unaofanyika katika halmashauri hiyo, hasa kwenye ujenzi wa miundombinu katika sekta ya Afya na Elimu, tofauti na halmashauri nyingine nchini.
"Ninafarijika sana kuleta fedha za miradi Arusha DC, kwa kuwa miradi inafanyika kwa viwango vya hali ya juu, serikali imeleta milioni 500 za kujenga kituo cha Afya Nduruma, mradi ukakamilika vizuri, ikaleta tena milioni 400 za kituo hiki cha Mbuyuni, nacho kimekamilika kwa wakati, majengo yako imara yakionesha wazi thamani ya pesa iliyotumika" amesema Waziri Jafo.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, licha ya kumshukuru Waziri Jafo na Serikalo ya awamu ya tano, inayoongozwa na Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri iliyotukuka ya usimamizi wa miradi katika halmashauri zote, amemuomba Waziri huyo, kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje 'OPD', hospitali ya wilaya ya Olturumet pamoja na wataalamu katika sekta ya afya ikiwemo, madaktari na wauguzi.
" Mheshimiwa Waziri, ili kukamilisha mikakati ya Serikali ya awamu ya tano, ya kusogeza huduma za afya kwa wananchi hasa waishio vijijini, na kupata thamani halisi ya majengo yote yaliyojengwa, ninakuomba utuletee watumishi wa sekta ya afya ili wananchi wa Arumeru waweze kutibiwa kwenye majengo haya mazuri" amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
Tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, halmashauri ya Arusha imepokea kiasi cha shilingi milioni 900, kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa Kituo cha afya Mbuyuni kwa shilingi milioni 400 na kituo cha Afya Nduruma kwa shilingi milioni 500, huku upatikanaji wa dawa thelathini muhimu na vifaa tiba ukifikia asilimi 90.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.