Watumishi wa makao Makuu, halmshauri ya Arusha, wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuzima moto, huku taasisi za Serikali, zikitakiwa kuchukua tahadhari, juu ya ajali zitokanazo na majanga ya moto kwa kufunga viashiria moto (Smoke Ditecto) pamoja na vifaa vya kuzimia moto (Fire Extinguisher) katika majengo yote ya taasisi hizo.
Tahadhari hiyo, imetolewa na askari wa kikosi cha Zima Moto na Uokoaji, wilaya ya Arumeru, Sajenti Babaa Toroso, wakati wa mafunzo hayo, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi za Makao Makuu, Halmashauri ya Arusha.
Sajenti Toroso, amesema kuwa, ni vema kuchukua tahadhari ya kufunga vifaa maalumu vya viashiria vya moto, vifaa vya kuzimia moto, pamoja na kujifunza namna ya kutumia vifaa hivyo, kwa lengo la kukabiliaba na majanga hayo ya moto.
Aidha Sajenti Toroso, amefafanua kuwa, asilimia kubwa ya hasara zinazosababishwa na majanga mengi ya moto, hutokana na watu kutokuwa na uelewa wa kutosha, juu ya umuhimu na matumizi ya vifaa vya kuzimia moto, pamoja na kushindwa kufuata utaratibu wa uzimaji moto.
Amesisitiza kuwa, kila jengo linapaswa kuwa na vifaa vya kuzimia moto 'fire extinguisher' , miundombinu rafiki ya kujikinga na majanga ya moto ikiwemo sehemu ya kusimama pindi moto unapotokea, pamoja na kutoa taarifa mapema pindi moto utakapotokea.
"Mara nyingi moto ukitokea, watu huanza kuzima kwanza, bila utalamu wowote, moto ukiwashindisha ndio wanaanza kutafuta Fire, jambo ambalo si sahii, pindi moto ukizuka, toa taarifa Fire kwa namba 114 bila gharama yoyote" amesema Sajenti Toroso.
Hata hivyo, watumishi wa halmashauri ya Arusha, wamelishukuru Jeshi hilo la Zima Moto, kwa kuwapa mafunza muhimu kwa jamii hiyo, kwani wengi wao, hawakuwa na ufahamu wa kutosha, juu ya tahadhari ya majanga ya moto na kuzima moto licha ya kuwa baadhi yao, humiliki na vifaa hivyo.
Awali, Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, linatoa elimu kwa jamii, ya namna ya kukabiliana na majanga ya moto na kuisisitiza jamii, kuchukua tahadhari kwani moto husababisha hasara na pengine vifo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.