Na . Elinipa Lupembe.
Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata, Jimbo la Arumeru Magharibi, wametakiwa kusimamia Kanuni, Sheria na taratibu za uchaguzi, kwa kutokujiingiza kwenye siasa, katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi mkuu, unaotegemea kufanyika tarehe 28 Oktaba, 2020.
Rai hiyo imetolwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule, wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata, mafunzo yanayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Maimamizi huyo ngai ya Jimbo, amewaasa Wasimamizi hao wasaidizi, kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria zinazoelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, taratibu ambazo zitawezesha kuwa na uchaguzi huru na haki kuanzia kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi na hatimaye siku ya uchaguzi mkui.
"Tunalo jukumu kubwa la kuhakikisha uchaguzi unasimamiwa kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za Uchaguzi, tumekula kiapo leo cha kutunza siri na kutokujihusisha na shughuli za chama chochote cha siasa, simamieni kanuni bila kuyumbishwa na mtu yoyote" amesisitiza Msimamizi huyo wa Uchaguzi.
Naye Afisa Sheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi Athmani Dunia, ameweka wazi kuwa mafunzo hayo ya siku tatu, yana lengo la kuwajengea uwezo na kuwa na uelewa wa pamoja, juu ya kuratibu na kutekeleza majukumu ya uchaguzi mkuu, majukumu yaliyokasimiwa kwao na serikali kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Hata Mwenyekiti wa mafunzo na Msimamizi Msaidizi ngazi ya kata, kata ya Nduruma, Loishuli Mollel, ameweka wazi kuwa wako tayari kupokea mafunzo, wanajiamiji na waka tayari pia kutekeleza majukumu hayo ya uchaguzi kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu za uchaguzi mkuu.
Jumla ya wasimamizi wasaidizi 54 wa uchaguzi ngazi ya kata, kutoka kata 27 za Jimbo la Arumeru Magharibi, wameanza kupata mafunzo ya Uchaguzi Mkuu, mafunzo yaliyoambatana na watalamu hao kula kiapo cha kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi mkuu kuelekea tarehe 28 Oktoba, 2020.
PICHA ZA MATUKIO
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule akifungua Mafunzo ya uchaguzi kwa Wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata, Mafunzo yanayofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Wasimamizi Wasaidizi ngai ya Kata Jimbo la Arumeru Magharibi, Wakisaini fomu za kiapo kabla ya kuanza Mafunzo ya Uchaguzi, yanayofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Afisa Sheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Athman Dunia, akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata, Jimbo la Arumeru Magharibi, wakati wa mafunzo kwenye ukumbi wa mkikutano, halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.