Na. Elinipa Lupembe.
Halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na shirika la Dorcas na Usharika wa Olokii, wameendelea kutoa elimu na hamasa juu ya tahadhari ya Kujikinga na gonjwa hatari la Corona kwenye maeneo ya vijiji na vitongoji vya kata za Mlangarini na Nduruma, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru.
Licha ya kutoa elimu hiyo, halmashauri kwa kushirikiana na wadau hao, wameendelea kuwasisitiza Wananchi kuweka ndoo za maji tiririka na sabuni kwenye milango ya Maboma yao ili kuhakikisha wageni wote wananawa mikono kabla ya kuingia ndani ya nyumba zao na pindi wanapotoka.
Aidha wazazi wamesisitizwa wanapoondoka nyumbani na kuwaacha watoto, wakumbuke kuwahimiza watoto wao, kunawa mikono kila wanapogusa vitu, wanawe mikono kadri wanavyoweza.
Zaidi wazazi wametakiwa kutokuwaruhusu watoto kuzurura hovyo pamoja na kuwafundisha na kuwasimamia watoto wao kuacha tabia ya kushika uso, kuweka mikono mdomoni, kuokota vitu kwani vitendo hivyo ni hatari kwa afya zao, vinaweza kuwasababishia maambikizi ya Corona.
Shime Watanzania wote tuungane kupambana na Gonjwa la Corona kwa Kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya na Wataalamu katika maeneo yetu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.