Na. Elinipa Lupembe.
Jumla ya Wanafunzi 7,018 waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka 2021, tayari wameanza mosomo rasmi, katika shule sekondari za serikali walizopangia baada ya kufaulu mitihani wa darasa la saba uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2020.
Afisa Elimu sekondari, halmashauri ya Arusha, Mwl. Menard Lupenza, amefafanua kuwa, jumla ya wanafunzi 7,018 sawa na asilimi 888, walio chaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule za sekondari za serikali za halamshauri ya Arusha, tayari wameripoti shuleni na kuanza rasmi safari yao ya masomo ya elimu ya sekondari.
Afisa Elimu Lupenza amefafanua kuwa jumla ya wanafunzi 7,886 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanaza mwaka 2021, wanafunzi 7, 018 tayari wamekwisharipotii kwenye shule walizopangiwa na kuanza masomo ya ya sekondari ambapo wasichana ni 3,153 na wavulana 2,746, na kuongeza kuwa kati ya hao, wanafunzi 607 wamehamia kwenye shule nyingine za serikali ndani na nje ya halmashauri ya Arusha.
"Kati ya wanafunzi 7,018, tumefuatilia idadi ya wanafunzi 512 wamekwenda kujiunga na shule za binafsi, na kama halmashauri tumejiridhisha na uandikishwaji wa wanafunzi hao kwenye shule za binafsi, lakini jumla ya wanafunzi 868, wasichana 432 na wavulana 436 sawa na asilimia 11, hawa bado hawajaripoti kwenye shule walizopangiwa, tunaendelea na utaratibu wa kuwatafuta kwa kushirikiana na maafisa watendaji wa kata na vijiiji na viongozi wa vijiji". Amefafanua Afisa Elimu huyo.
Naye mkuu wa shule ya sekondari Oldonyowas, mwalimj Richard Mugabuso amethibitisha kupokea jumla ya wanafunzi 67 kati ya wanafunzi 83 waliopangiwa, na kuongeza kuwa, jumla ya wanafunzi 63 walihamia kutoka shule nyingine walizopangiwa na wanafunzi 12 wamehama kwenda shule nyingine na sekondari, huku wanafunzi 4 tu hawajaripoti shuleni hapo.
Hata hivyo mkuu wa shule ya sekondari Mukulat, mwalimu ...naye amethibitisha kupokea jumla ya wanafunzi 279 wavulana 117 na wasichana 163 kati ya wanafunzi 300, waliopangiwa shuleni hapo kuanza masomo ya sekondari Januari mwaka 2021.
Wakati huo huo mchakato wa kuendelea na ujenzi wa kukamilisha ujenzi wa vyumba 52 vya madarasa, wakati vyumba 42 viko hatua za ukamilishaji, vyumba 5 viko kwenye hatua ya lenta, vyumba 4 viko kwenye kupandisha kuta na chumba 1 kiko kwenye hatua ya msingi.
Uongozi wa halmashauri ya Arusha, unawataka wazazi na walezi ambao hawajawawezesha watoto wao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021, kuhakikisha wanafunzi hao wanarepoti kwenye shule walizopangiwa, na kushindwa kufanya hivyo, seriakli itawachukulia hatua za kisheria.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.