Na Elinipa Lupembe.
.Vijana shule ya sekondari Mukulat, halmashauri ya Arusha, wamekiri kuwa na ndoto na malengo makubwa katika maisha yao ya sasa na yajayo, lakini wametambua vikwazo na changamoto zinazokwamisha ndoto hizo ni pamoja na uelewa mdogo juu ya mabadiliko yao binafsi ya kimwili na kitabia yanayotokana na makuzi yanakuwa ni kikwazo kwa vijana wengi katika kufikia ndoto na malengo yao.
Wakizungumza wakati wa mdahalo juu ya afya ya uzazi kwa vijana, uliofanyika shuleni shuleni hapo mwishoni mwa wiki ukishirikisha watalamu na wanafunzi, vijana hao wameainisha baadhi ya changamoto na vikwazo, vinavyochangia kupotez andoto na malengo ya vijana wengi nchini ni pamoja na mimba na ndoa za utotoni kwa wasichana, uvutaji wa bangi, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na ulevi katika umri mdogo, mambo ambay ni sugu na yanasababisha vijana wengi kutokufikia ndoto na malengo yao.
Hata hivyo vijana hao wamefafanua kuwa licha ya kuzitambua changamoto hizo, wanahitaji mbinu salama za kukabiliana nazo, huku wavulana wakisistiza uhitaji mkubwa wa mbinu za kukabiliana na mihemko ya ujana ili kuepuka kujiingiza wao na kushawishi wasichana kujiingiza kwenye ngono katika umri mdogo.
Denis Laurance, mwanafunzi wa kidato cha 3, amefafanua kuwa, elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana inahitajika sana kwa vijana na kuongeza kuwa wao, wameanza kujitambua mara baada ya kupata fursa ya kushiriki mafuzno yanayotolewa shuleni hapo pamoja na kutumia program ya Huduma Rafiki kwa Vijana inayotolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, huduma ambayo imekuwa ni suluhisho kwa vijana wengi sasa.
"Tunapofundishwa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana, inyotupa mbinu ya kukabiliana na mabadilikonya kimwili katika makuzi yanayopelekea mihemko na hisia, inatusaidia kukabiliana na changamoto hizo na tunamiini vijana wengi sasa watatimiza ndotozao tofauti na hapoa awali"amesema Denis.
Halmashauri ya Arusha kwa kushirikia na na shirika la Jhepeigo Tanzania inatekeleza mradi wa Afya ya Uzazi kwa vijana na Huduma Rafiki kwa Vijana, kwa ufadhili wa mfuko wa Bill&Melinda Gate wa nchini Marekani, umekuwa chachu ya mabadiliko chanya ya kitabia kwa vijana wa kisasa wa halamshauri ya Arusha.
YOUTH to the moon
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.