Afisa Mwandikishaji, Jimbo la Arumeru Magharibi, anawatangazia Wananchi wote kuwa, Uboreshaji wa Daftati la kudumu la Wapiga Kura Awamu ya pili, utafanyika kwa siku tatu, kuanzia tarehe 17 hadi 19/04/2020.
Wapiga Kura wote wanatakiwa kwenda kuhakiki taarifa zao, kwenye Vituo Vilivyoainishwa kwenye Kata zao.
VITUO VITAFUNGULIWA KUANZIA SAA 08:00 Asubuhi mpaka saa 12:00 jioni.
ZOEZI LA UANDIKISHAJI LITAHUSISHA : —
Kuandikisha wapiga Kura Wapya waliotimiza umri wa miaka 18 na zaidi, na wale watakaotimiza umri huo ifikapo siku ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
Kuandikisha wale wote wenye sifa lakini hawakujiandikisha katika uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura awamu ya kwanza.
Kutoa Kadi mpya kwa Wapiga Kura waliopoteza kazi zao
Kuhamisha taarifa za Wapiga Kura waliohama Kata au Jimbo la Uchaguzi na kuhamia katika eneo jingine.
Kurekebisha taarifa za Wapiga Kura ambazo zilikosewa
Kuondoa Wapiga Kura waliopoteza sifa kama vile kufariki.
UTARATIBU WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI.
Kila Kata kutakuwa na Kituo Kimoja, Mwandishi Msaidizi na BVR KITs ambayo itakuwa na Orodha ya majina ya Vituo vyote vilivyoandikishwa awamu ya kwanza.
Mpiga kura yeyote anaweza kuboresha taarifa zake kwa kuzingatia kituo anachotaka kupiga kura siku ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
KUMBUKA: SIFA MUHIMU ZA KUKUWEZESHA KUPIGA KURA SIKU YA UCHAGUZU MKUI MWA 2020 NI KUWA NA KADI YA MPIGA KURA.
*****Kadi yako kura yako, nenda kajiandikishe*******
MUHIMU: KUMBUKA KUZINGATIA KANUNI ZA AFYA KWA KUFUATA Maelekezo utakayopewa Kituoni, ili kuepusha maambukizi ya Virus vya CORONA.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.