Na. Elinipa Lupembe.
Katika kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu na kurejesha kiwango cha taaluma kwenye shule za serikali na kumuwezesha mtoto wa kitanzania na kupata elimu bila malipo, kwenye mazingira bora, Serikali sasa imezigeukia shule kongwe.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Ufundi, imejipanga kufanya ukarabati kwenye shule 62 kongwe, shule ambazo zilikuwa zimetelekezwa na kupotea kwenye ramani ya shule bora Tanzania na kupoteza hadhi ya shule hizo iliyokuwepo kwa miaka ya nyuma.
Mradi huo mkubwa ambao haujawahi kutokea kwa miongo kadhaa nchini, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Magufuli, imewekeza kiasi cha shilingi bilioni 308.1, kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa maabara na nyumba za walimu kwa shule zote 62.
Ikumbukwe kuwa, mradi huo mkubwa ni utekelezaji Ilani ya Chama cha Mapinduzi, kupitia ahadi ya Elimu bila malipo, iliyotolewa na mheshimiwa Rais, wakati akiingia madarakani miaka minne tu iliyopita, mwaka 2015.
Shime watanzania tuendelee kuunga mkono juhudi za Serikali yetu ya awamu ya tano, na rais wetu, katika utekeleza majukumu ya nchi yetu, kwa maendeleo ya watanzani masikini wanaosoma kwenye shule za Serikali.
#Tumejipanga#Tunatekeleza#Hapa Kazi tuu#
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.