Na. Elinipa Lupembe.
Wafugaji wa ng'ombe wa maziwa, wametakiwa kubadili mtazamo na kuanza kufuga kibiashara kwa tumia teknolojia ya kisasa ya Uhimilishaji, teknolojia ambayo ni mkombozi na imeleta mapinduzi makubwa kwa wafugaji wengi kwa kufuga ng'ombe bora wa maziwa, wenye kuongeza pato la mfugaji.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kwenye viwanja vya maonesho ya Wakulima Kanda ya Kaskazini, ndani ya Banda la Mifugo, halmashauri ya Arusha, Daktari wa Mifugo halmashauri hiyo, Dkt. Yohana Kiwone, ameanza kwa kueleza kuwa, ili wafugaji waweze kujikomboa kiuchunmi wanatákiwa kufuga kisasa, ufugaji utakaowaongezea kipato, ni vema kutumia teknolojia ya uhimilishaji, teknolojia inayomuwezesha mfugaji kuchagua mbegu bora ya ng'ombe, ng'ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa mengi, nyama nyingi na ngozi bora kwa biashara na viwanda.
Amefafanua kuwa teknolojia ya uhimilishaji, ni teknolojia inayoruhusu ng'ombe kumpandikizwa bila dume, na kupata mbegu bora ya ng'ombe, mwenye uwezo wa kutoa lita 20 mpaka 30 za maziwa kwa siku, na kumuwezesha mfugaji kuchagua aina ya ng'ombe anayemtaka na jinsia ya ng'ombe anayotaka.
Hata hivyo ameweka wazi kuwa teknolojia ya uhimilishaji, imeleta mapinduzi makubwa katika uzalishaji wa maziwa hasa kwa wafugaji wanaofugia ng'ombe ndani, wengi wamepata mafanikio makubwa kwa kubadili uzao wa ng'ombe wao, na ng'ombe hao kuzaa ng'ombe bora wenye kutoa maziwa mengi, jambo ambalo limewaongezea kipato kwa sasa, tofauti na hapo awali.
"Kuelekea uchumi wa viwanda, mfugaji anatakiwa kuachana na kufuga kienyeji, badala yake afuge kisasa, mifugo itakayotoa mazao yenye ubora kwa matumizi ya viwanda, teknolojia ya uhimilishaji pekee, ndio teknolojia inayoweza kumfanya mfugaji kupata rasilimali za kuweza kuendesha viwanda vinavyotengeneza bidhaa zitokanazo na maziwa" amesisitiza Dkt. Kiwone.
Aidha amefafanua kuwa, endapo mfugaji atakuwa na ng'ombe bora anayetoa wastani wa lita 20 kwa siku, anauwezo wa kupata shilingi elfu 20 kwa siku, na shilingi laki 6 kwa mwezi, huku akiwa na uhakika wa kupata nyama na ngozi bora pindi ng'ombe huyo atakapofikisha umri mkubwa wa kukoma kuzaa.
"Kiasi cha shilingi laki 6 kwa mwezi ni kisio la chini kwa mfugaji anayenza na ng'ombe mmoja, lakini mfugaji akiwa na ng'ombe watano anaweza kupata shilingi laki 1 kwa siku, kwa mwezi ni shilingi milioni 3 na kwa mwaka ni milioni 36, biadhara ambayo itamkomboa mfugaji na kuimarisha uchumi wake binafsi na uchumi wa Taifa.
Kwa sasa wafugaji wa ng'ombe Halmashauri ya Arusha, waliotumia teknolojia ya uhimilishaji wameanza kuona na mafanikio ya teknolojia hiyo, kumwkuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji kwa mwaka 2019/2020 jumla ya ng'ombe 3,538 wamezaliwa ikiwa ni wastani wa ng'ombe 295 kwa mwezi.
Teknolojia hiyo ya uhimilishaji inapatikana kwenye viwanja vya maonesho ya wakulima Njieo, fika kwenyw Banda la mifugo halmashauri ya Arusha, na baada ya maonesho fika ofisi za Mifugo halmashauri ya Arusha eneonla Sekei, utapata huduma hiyo, shime wafugaji tuchangamkie fursa hiyo.
'Tanzania ya Viwanda iko mikononi mwetu'.
"KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI, CHAGUA VIONGOZI BORA 2020"
PICHA ZA BANDA LA MIFUGO ARUSHA DC
Daktari wa Mifugo halmashauri ya Arusha, Dkt. Yohana Kiwone akimuelezea ng'ombe aliyezaliwa kwa teknojia ya Uhimilishaji, ng'ombe ambaye anatoa lita 20 za maziwa kwa siku akiwa tayari ana mimba ya miezi 3.
Ng'ombe waliozaliwa kupitia teknolojia ya Uhimilishaji, wakiwa kwenye Banda la Mifugo halmashauri ya Arusha kwenye maonesho ya wakulima Kanda ya kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi- Njiro Jijini Arusha.
Ng'ombe bora wa maziwa mwenye uzito mkubwa na mwenye uwezo wa kutoa maziwa lita 20 mpaka 30 kwa siku.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.