• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

SERIKALI KUNUSURU WASICHANA SEKONDARI EINOTI NA NDOA ZA UTOTONI

Posted on: June 17th, 2020

Na. Elnipa Lupembe.

     Serikali ya awamu ya tano, imeendelea kuweka mipango thabiti ya kumlinda mtoto wa kike kwa kuweka mazingira rafiki ya shuleni, ili kumuwezesha kusoma bila kubughudhiwa na changamoto za kijamii ikiwemo mimba na ndoa za utotoni, zinazomkabili mtoto wa kike katika kipindi cha masomo,lengo likiwa ni kupandisha kiwango cha taaluma na kuongeza ufaulu kwa wasichana.

    Juhudi hizo zimefanywa na Serikali kupitia, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 75 za kujenga bweni la wasichana shule ya Sekondari Einoti kata ya Kisongo, halmashauri ya Arusha.

     Akizungumza na mwandishi wetu, Mkuu wa shule ya sekondari Einoti, Mwalimu Justine Swai, ameeleza kuwa, licha ya kuwa uwepo wa bweni la wasichana shuleni hapo kupandisha kiwango cha taaluma na ufaulu kwa wanafunzi wasichana, utasaidia pia kuwaepusha watoto wa kike na changamoto za kijamii, zinazowakabili kutokana na mila na desturi za jamii za wafugaji, ikiwemo mimba na  ndoa za utotoni pindi wanaporudi nyumbani kila siku.

     "Katika jamii za wafugaji, elimu kwa mtoto wa kike sio kipaumbele, zaidi huandaliwa kwa ajili ya kuolewa, na mara nyingi hukosa muda wa kujisomea awapo nyumbani, kutokana na kupangiwa kazi za kufanya kila siku arudipo nyumbani, tofauti na mtoto wa kiume jambo ambalo linawarudisha nyuma kitaaluma na kushindwa kufanya vizuri kimasomo sawa na watoto wa kiume" ameleza Mkuu huyo wa shule.

       Hata hivyo mwalimu Swai, amefafanua kuwa, kutokana na changamoto za mimba na ndoa za utotoni, shule iliamua kuanzisha madarasa mawili kutumika kama hosteli za wasichana, wenye changamoto za kijamii zinazofanywa na jamii za wafugaji,jaribio ambalo lilileta mafanikio kitaaluma na kijamii kwa wasichana shuleni hapo.

    Aidha,  Mkuu huyo wa shule, ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga bweni la wasichana shuleni hapo, kwa kuwapunguzia kutembea umbali mrefu kutoka nyumbani, jambo litakalomfanya mwanafunzi kupata muda mrefu wa kujisomea na kujiepusha na mazingira hatarishi.

     Afisa Elimu sekondari halmashauri ya Arusha, Menard Lupenza amesema kuwa, ujenzi wa bweni hilo la wasichana, unategemea kuwa na matokeo mazuri kitaaluma kwa wanafunzi hao, kutokana na kuishi katika mazingira bora jambo ambalo litarahisiha tendo la kujifunza kwa wanafunzi hao.

     Ameongeza kuwa, lengo la serikali,  ni kuweka mazingira bora ya kujifunzia kwa watoto wa kike, na kuwaepusha na changamoto za kijamii zinazowakabili kwa kuwawezesha kusoma kwa bidii bila kubughudhiwa, na kuwataka wasichana kutumia fursa hiyo muhimu kipindi chote wawapo shuleni.

      Hata hivyo, Afisa Elimu huyo amefafanua kuwa, kiasi hicho cha fedha, kimejenga bweni moja lenye vyumba 22, ofisi ya matroni, vyoo na mabafu na sehemu ya kufulia, bweni ambalo litakalolaza wasichana 80, na linategemea kukamilika mapema mwezi Septemba.

    Shule ya sekondari Einoti ina jumla ya wanafunzi 763, wavulana 276  na wasichana 485 na inafanya vizuri kitaaluma kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 ilishika nafasi ya pili ngazi ya halmashauri ya Arusha.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DKT. PASCAL KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 19, 2025
  • WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

    June 17, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.