Na. Elinipa Lupembe.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF wameanza ujenzi wa mabweni, mawili ya wasichana shule ya sekondari mabweni Oldonyowas, kuokoa wasichana, kuondoka na ndoa za utotoni kwa kujenga mabweni
Wakizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa mabweni, wasichana wa shule hiyo, wamesema kuwa, uwepo wa mabweni utawasaidia wasichana wengi wa jamii ya wafugaji kuondokana na changamo ya ndoa za utotoni, zinazowakabili kutokana na mila na desturi za jamii hiyo.
Wamesema kuwa, wasicha wengi wa jamii ya wafugaji, wamekosa nafasi ya kuendelea na masomo na kukatisha ndoto zao, kutokana na mila na desturi zinazowasababisha, kuacha masomo na kuolewa na wengine kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo kutokana na kazi nyingi wanazofanya mara baada ya kutoka shuleni.
Malkia Losiyeku, mwanafunzi wa kidato cha kwanza, shule ya sekondari Oldonyowas, amethibiyisha kuwa, uwepo wa mabweni ya wasichana, utawaepesha na mambo mengi ya mila na desturi yanayoendelea nyumbani, ikiwemo kuachishwa masomo na kuozeshwa katika umri mdogo.
Amesema kuwa anaamini, wasicha wakiwa bweni, watakuwa chini ya usimamizi salama wa walimu, usimamizi ambao utawafanya wazazi kuogopa kuwaondoa watoto na kwenda kuwaozesha kwa kuhofia watoto hao wako chini ya serikali.
Heavenligh Geophray amesema kuwa, uwepo wa mabweni ya wasichana, utawezesha ufaulu kwa kuwa wasichana wengi hukosa muda wa kujisomea nyumbani kutokana na wasichana kutumia muda mwingi kufanyakazi wanazopangiwa kufanya kila siku jioni, mara watokapo shuleni.
"Ukirudi nyumbani jioni, unatakiwa kwenda kuchota maji, kutafuta kuni, kupika, ukimaliza kazi hizo unakuwa tayari umechoka, huwezi hata kusoma tena, na asubuhi unatakiwa kuamka alfajiri kuwa shule, unakwenda shule umechoka na kurudi umechoka"amesema Heavenlight.
Ameongeza kuwa, wanafunzi wengine wanaishi mbali sana na shule, wanapita kwenye mapori na makorongo, mazingira ambayo ni hatarishi kwa wasichana, kuweza kufanyiwa vitendo vya ukatili, lakini uwepo wa mabweni, utasaidia kuepusha madhara ambayo yanaweza kumpata msichana njiani.
Hata hiyo mkuu wa shule ya Oldonyowas, mwalimu Richard Mugabuso, amethibitisha kuwa, ujenzi wa mabweni hayo ni muhimu kwa wasichana ambao wanachangamoto nyingi nyumbani na shuleni, hivyo wepo wa bweni, utawezesha wasichana kupata muda wa kujisomea, kuongeza ufaulu pamoja na kupandisha kiwango cha taaluma shuleni hapo.
Ana Lukas, mzazi mwenye mtoto wakike shuleni hapo, ameishukuru serikali kupitia TASAF kwa mradi huo wa mabweni, na kusema kuwa wasichana kukaa shuleni kutaleta amani hata kwa wazazi, kwani mtoto akienda shule, mzazi hukosa amani na kuwaza pengine atakutana na majaribu gani njiani.
Ujenzi wa mabweni mawili ya wasichana, shule ya sekondari Oldonyowas, uko kwenye hatua za awali na unatekelezwa na serikali kupitia miradi ya uboreshaji miundombinu, miradi inayotekelezwa na TASAF awamu ya III, kwa gharama ya shilingi milioni 144.7, mabweni yanayotegemea kulaza wasichana 96, ikiwa wanafunzi 46 kwa kila bweni.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.