Madiwani wa kata 27 za halmashauri ya Arusha wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za kata zao kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni 2017 katika Mkutano wa Baraza la kata uliofanyika kwenye Ukuùmbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha.
Katika mkutano huo madiwani waliwasilisha taarifa mbalimbali za kata ikiwemo taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye kata zao, taarifa za Fedha yaani mapato na matumizi, taarifa za Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Miundombinu ya barabara, Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii, hali ya chakula katika kata pamoja na taarifa za ulinzi na usalama.
Taarifa hizo zinaonyesha taswira halisi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo za halmashauri na pia zinaiwezesha halmashauri kufanya tathmini ya hali halisi pamoja na kupanga mikakati thabiti ya kufikia malengo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.