Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, Dkt. Wilson Mahera, anawatangazia wananchi wote, kuungana na watu wote duniani, kushiriki maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yatakayofanyika tarehe 18.06.2019, kwenye viwanja vya shule ya Msingi Ngaramtoni kata ya Olturumet, kuanzia saa 02:30 asubuhi.
Maadhimisho hayo yataambatana na shughuli mbalimbali zitakazofanywa na watoto wenyewe, ikiwemo maandamano yatakayoongozwa na Mgeni Rasmi, pamoja na burudani zilizobeba jumbe mbalimbali zinazohusu Haki, Wajibu na Maendeleo ya Mtoto wa Afrika.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.