Na. Elinipa Lupembe.
Serikali imeahidi kutafuta fedha nyingine, kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa miundombinu ya shule ya sekondari Ilboru, ikiwemo baadhi ya vyumba vya madarasa, mabweni, vyoo na mabafu pamoja na nyumba za walimu, miundombinu iliyojengwa kabla ya kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika.
Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI, Mheshimiwa Mwita Waitara, alipotembelea shuleni hapo, kukagua utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa shule hiyo ya sekondari Ilboru, uliofanywa na serikali kupitia fedha zilizotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania - TEA za ukarabati wa shule kongwe nchini.
Naibu Waziri huyo ametoa ahadi hiyo, baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya kwanza,mmradu ambao licha ya kukamilika kwa fedha zilizotolewa lakini bado shule hiyo kongwe, inahitaji ukarabati kwenye miundombinu ambayo haikufikiwa wakati wa awamu ya kwanza ya ukatabati wa shule hiyo, ikiwemo mabweni, baadhi ya vyumba vya madarasa na nyumba za walimu, mradi unaotegemea kugharimu shilingi milioni 900.
"Kwa hali niliyoiona ya majengo ya zamani, na taarifa mliyonipa, kunauhitaji wa ukarabati wa miundombinu iliyobaki, tunakwenda kuangalia namna ya kuingiza shule ya Ilboru kuweza kupata fedha, milioni 900 za kumalizia ukarabati huo, ni kweli majengo yamechoka kutokana na kujengwa miaka mingi iliyopita". amefafanua Naibu Waziri huyo.
Hata hivyo Naibu Waziri, amewasihi viongozi wote kuanzia ngazi ya wilaya, halmashauri na shule pindi watakapopata fedha hizo, kutumia forced account na mafundi wazawa 'local fundi', pamoja na kuzisimamia fedha hizo kwa karibu na umakini ziweze kukamilisha ukarabati huo, kwenye maeneo yaliyobaki.
Ameweka wazi kuwa, licha ya kukamilika awamu ya kwanza ya ukarabati iliofanyika kweye shule 86 nchini, Serikali imejipanga kuanza kufanya ukarabati wa shule za kawaida na zile za kata, mara baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ukarabati wa shule zake kongwe, ikiwmo shule ya sekondari Ilboru.
Naye Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, amemuahidi Naibu Waziri huyo, kusizimamia fedha hizo na kukahikisha zinatumika kulingana na maelekezo ya serikali, mara tuu serikali itatekeleza ombi lao, la kumalizia ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo iliyobaki, ikiwemo nyumba za walimu.
"Mheshimiwa Naibu Waziri, tunakushukuru na tunakupongeza wewe na serikali, serikali makini nayoongozwa na Jemadari, Rais wetu Dkt. John Magufuli, kwa kuijali wilaya ya Arumeru, wilaya hii ni moja ya wilaya inayopendelewa kwa kupata fedha nyingi za miradi hasa katika sekta hii ya elimu na afya, nikuahidi kuendelea kusimamia matumizi sahihi ya fedha yoyote ya serikali, itakayoletwa katika wilaya yangu". amesisitiz mkuu huyo wa Wilaya.
Naye mkuu wa Shule ya sekondari Ilboru, amesema kuwa shule ya sekondari Ilboru, ni shule moja ya shule kongwe nchini inayofanya vizuri kitaaluma, ilianza rasmi mwaka 1946 kabla ya Uhuru wa Tanganyika, ikiwa sasa na jumla ya wanafunzi 817 wavulana, na ina jumla ya vyumba vya madarasa 18.
PICHA ZA MATUKIO ZIARA YA NAIBU WAZIRI ILBORU SEKONDARI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.