Na. Elinipa Lupembe.
Halmashauri ya wilaya Arusha imepokea msaada wa vifaa tiba vya mifugo, kutoka shirika lisilo la kiserikali la OIKOS, shirika linalofanya shughuli zake ndani ya halmashauri hiyo, kwa kujihusisha zaidi na masuala ya Ardhi, Kilimo na Mifugo, kupitia mradi wa Eco - Boma, mradi unaofadhiliwa na nchibza Ulaya.
Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Dkt. Wilson Mahera, ameushukuru uongozi wa shirika hilo kwa jitihada wanazofanya hasa katika kuwajengea uwezo wananchi wa halmashauri hiyo, shughuli ambazo ni msingi wa maendeleo kwa jamii ya wananchi wa halmashauri hiyo na taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa anatambua na kuthamini, mchango mkubwa unaotolewa na shirika la OIKOS, mchango ambao unaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano, kutokana na kazi zinazofanywa na shirika hilo, kazi ambazo zinaonekana wazi, kuwafikia wananchi wa hali ya chini na kuongeza, kuwa kazi hizo zina matokeo chanya kwa wananchi.
Aidha amewataka maafisa Ugani, kutumia vifaa hivyo kwa lengo lililokusudiwa, la kuwahudumia wafugaji na kuongeza kuwa ni vema maafisa Ugani hao kuwafuata wafugaji, katika maeneo yao na si kuwasubiri ofisini mpaka wafugaji wawatafute, huku akiwasisitiza kutoa huduma kwa weledi kwa kuzingatia sheria na kanuni zinavyoelekeza.
"Ninataka vifaa hivi vitumike kutoa huduma stahiki kwa wafugaji na si vinginevyo, na zaidi wafuateni wafuga kwenye maeneo yao na si kuwasubiri wawafuate ofisini,toeni huduma kwa weledi huku mkizingatia kanununi na taratibu zinavyoelekezwa" amesema Kurugenzi Mahera.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Meneja msaidizi mradi wa Eco Boma unaotekelezwa na shirika la OIKOS, Ifura Ukio amesema kuwa lengo la kutoa vifaa huvyo kwa halmashauri ni kuwawezesha maafisa ugani kutoa huduma ya chanjo kwa mifugo kwa urahisi, chanjo ambazo zitazuia magonjwa ya mifugo na kuimarisha afya ya mifugo.
Amesema kuwa shirika linatambua na kuthamini juhudi za serikali za kuimarisha zao la mifugo kuelekea uchumi wa viwanda, hivyo kuamua kuwawezesha watalamu kutoa huduma ya chanjo kwa ufanisi zaidi.
Ifura amevitaja vifaa vilivyokabidhiwa kwa halmashauri hiyo ni pamoja na Freezaer moja kwa ajili ya kuhifadhia chanjo, cool box 10, tano za ujaxo wa lita 10 na tano za ujazo wa lita tano kwa ajili ya kubebea chanjo kutoka kwenye stoo ya chanjo kwenda kwa wafugaji, pamoja na kutengeneza fiji kubwa ya halmashauri ambayo ilikuwa imeharibika.
Naye Daktari wa Mifugo halmashauri ya Arusha Dkt. Linus amesema kuwa uwepo wa vifaa tiba hivyo utarahisisha kazi ya chanjo kwa Maafisa Ugani kwenye kata na vijiji, kutokana na ukweli kuwa ukosefu wa vifaa tiba.
Amefafanua kuwa, awali Maafisa Ugani walikuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa vifaa tiba, jambo ambalo liliwalazimu baadhi ya Maafisa Ugani, kukodi au kununua cool box ndogo ili kuwezesha zoezi hilo la kutoa chanjo kwa mifugo huku wengine wakishindwa kumudu kununua vifaa hivyo.
Hata hivyo vifaa tiba hivyo vitagawiwa kwenye ofisi za kata, kwa ajili ya kurahisishia Maafisa Ugani wa vijiji utoaji wa chanjo kwenye vijiji kwa wafugaji wenye mifugo inayopatiwa chanjo za magonjwa ambayo chanjo zake hutolewa kila baada ya miezi mitatu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.