Na. Elinipa Lupembe.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Dkt. Godwin Mollel, ameuagiza uongozi wa wilaya ya Arumeru, kutambua mchango unaotelewa na taasisi za dini katika sekta ya afya kwa kuweka mpango wa pamoja katika kuhudumia watoto wenye matatizo ya ulemavu nchini.
Naibu Waziri huyo, amesema hayo, alipotembela The Plaster House, inayoendeshwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzanzia Dayosisi ya Kaskazini Kati, chini ya hospitali ya Seliani Ngaramtoni, na kushudia huduma mbalimbali za upasuaji zinazotolewa kwa watoto wenye ulemavu wa viungo na kurekebishwa viungo hivyo na kuwa wazima kuendelea na maisha ya kawaida.
Nimejionea kazi inayofanyika hapa Plaster House, kazi inayofanyika ni kubwa ya kuisaidia watoto wa kitanzania wenye ulemavu kwa gharama za wafadhili, ifike wakati sasa Serikali kuanza kufikiria namna ya kuweka mipango ya kushiriana na Plaster hii, kuwahudumia watoto wenye changamoto za ulemavu nchini, ambao wengi wao wanafichwa na kukosa haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kupata elimu." amesema Naibu Waziri huyo.
Amemtaka Mkuu wa wilaya ya Arumeru, kuangalia namna ya kuweka mipango ya kuongeza nguvu kwenye Plaster House hiyo, Plaster ambayo kimsingi inatoa huduma kubwa mno kwa wananchi wasio na uwezo kiuchumi, huduma ambayo ingepaswa kutolewa na serikali, hivyo ameagiza halmashauri kutambua umuhimu wa huduma hiyo na kuweka mkakati wa kushiriki kwa hali na mali kuisaidi utoaji wa huduma hiyo na kufikia watoto wengi zaidi wenye ulemavu.
Naye mkuu wa wilaya ya Atumeru Mhe. Mhandisi Richard Ruyango, licha ya kuridhishwa na huduma za upasuaji zinazotolewa na Plaster House hiyo, ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Plaster House hiyo kupitia kanisa l KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, na kuahidi kukutana na uongozi wa Kituo hicho kupanga namna ya serikali kushiriki katika kuongeza utoaji wa huduma hiyo kupitia halmashauri ya Arusha na wadau wengine wa maendeleo.
Akielezea shughuli zinazofanya na kituo hicho Mratibu wa Mradi Aireen Ulomi, amefafanuwa kuwa The Plaster House hiyo inafanya upasuaji wa kurekebisha ulemavu wa aina mbalimbali kwa watoto wa chini ya miaka 18, ikiwemo 'neuro surgery' kwa wenye matatizo ya migongo wazi na vichwa vikubwa, 'orthopedic surgery' kurekebisha mifupa kwa watoto wenye matege makubwa wanaoshindwa kutembea na miguu kifundo, 'plastic surgery' kwa watoto waliopata majanga ya moto na kusababisha ulemavu, pamoja na watoto wenye midomo sungura.
Aidha Aireen ameongeza kuwa, huduma zote hizo zinatolewa kupitia wafadhili kutoka ndani na nje ya nchi hasa nchi za Marekani na Australia, huku wazazi wakichangia kiasi kidogo cha gharama, kwa ajili ya matibabu, ikiwa na lengo la kuweka ushirikiano kati Plaster na familia za watoto wanaopata huduma
"Plaster House ina uwezo wa kuhudumia mpaka watoto 140 kwa wakati mmoja. na kwa mwaka tunahudumia zaidi ya watoto 700, kutoka maeneo yote nchini Tanzania, katika kipindi chote cha matibabu mtoto hukaa kituoni hapa, huku akiendelea kupata huduma ya kufundishwa stadi mabalimbali ili akimaliza kutibiwa aende akaanze shule, kupitia mfumo rasmi wa elimu" ameweka wazi Mratibu huyo wa Plaster House
Aidha ameelezea licha ya mafanikio ya huduma ya matibabu wanayopata watoto, lakini pia baada ya matibabu watoto hao huweza kumudu kuanza masomo kama watoto wengine, kutoka na ukweli kwamba jamii nyingi bado zina unyanyapaa kwa watoto walemavu, wengi wanaofika hapo wanakuwa hawajapelekwa shule kutokana na mtazamo hasi wa jamii juu ya ulemavu.
Hata hivyo imelezwa kuwa licha ya jitihada za serikali na wadau mbalimbali kushiriki kutoa huduma hizo lakini bado jamii inakabiliwa na changamoto ya kuwaficha watoto watoto wenye ulemavu na baadhi kukataa kugharamia kiasi kidogo ili kuwaleta watoto kupata huduma, na kuwaona kwamba hawana umuhimu tena katika jamii, jambo ambalo kupitia mradi huu, unawatafuta watoto hawa na kuwaelimisha wazazi katika maene yao.
Awali KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kapitia programu yake ya The Plaster House chini ya Hospitali ya Selian Ngaramtoni, imefanikiwa kutoa hudumia takribani watoto 5,000 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 ikiwa na uwezo wa kuhudumia mpaka watoto 140 kwa wakati mmoja, na wastani wa zaidi ya watoto 700.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri, alifanya ziara katika hospitali ya mkoa wa Arusha Mount Meru, hospitali ya Lutherani Selian Hospital za jijini Arusha pamoja na Hospitali ya wilaya ya Arusha Olturumeti na hospitali ya Serilin Ngaramtoni inayosimamia kituo cha The Plaster House na kuzungumza na watumishi wa hospitali hizo zote.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.