*MWAKA MMOJA WA DC MURO ARUMERU*
*SEKTA YA ELIMU*
Ndugu zangu wana *Arumeru* kama mtakumbuka nilipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru *Tarehe 28/07/2018* Wilaya yenye Halmashauri mbili, Arusha Dc na Meru Dc zenye jumla ya tarafa 6 na *kata 53* Zenye Majimbo mawili ya Arumeru Mashariki na Magharibi Moja kati ya kazi niliyoanza nayo ni kuanzisha *kampeni ya ujenzi wa madarasa 107* mapya kwa ajili ya shule za sekondari na msingi ujenzi ambao unagharimu zaidi ya *Shilingi Bilioni 2 * na sasa tumeweza kujenga vyumba vya *madarasa 149* badala ya 107
*Leo nimeona busara* kuwaletea mrejesho wa kampeni hii ambayo imefikisha mwaka sasa kama ifuatavyo;
*1. Katika Halmashauri ya Meru* Vyumba 35 vya madarasa ya shule za msingi na Sekondari vimekamilika,
Vyumba 42 vya madarasa ya sekondari na msingi vipo kwenye hatua za mwisho kukamilika, pia tumejiongeza kwa kujenga majengo ya Utawala mawili (2) hatua ya ukamilishaji, pamoja na Maabara mbili (2) za science zipo hatua ya uezekaji.
Pia tumekamilisha ujenzi wa jengo jipya na la kisasa la wadhibiti ubora wa Elimu.
*Hivyo katika Halmashauri ya Meru tumeshajenga vyumba na majengo 82 *
*2. Halmashauri ya Arusha*
Madarasa yaliyokamilika 34 ambayo yameanza kutumiwa kwa ajili ya sekondari na msingi na yaliyo katika hatua ya mwisho ni madarasa 73 kwa ajili ya shule za msingi na sekondari, katika Halmashauri ya Arusha jumla ya Madarasa 107 yanajengwa katika kampeni hii.
*MAFANIKIO YETU*
*1. Kampeni yetu ya madarasa mpaka sasa inatupa fursa ya kuwa na jumla ya vyumba vya madarasa 149 kutoka malengo ya kujenga vyumba 107*, hivyo tumevuka lengo kwa zaidi ya asilimia
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.