Na. Elinipa Lupembe.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi Saad Mtambule , amemkabidhi fomu za Uteuzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi , Mchungaji Wilson Loilole Laiser kupitia chama cha NCCR- MAGEUZI.
Mchungaji Wilson Laiser, kupitia Chama cha NCCR - Mageuzi , aliwasili majira ya saa 05:50 asubuhi, kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo, eneo la Sekei, akiwa ameambatana na Mwenyekiti na Katibu wa Chama hicho wilaya ya Arumeru pamoja na wajumbe wengine wa chama hicho, na kukabidhiwa fomu hizo za Uteuzi mnamo saa 12:12 mchana, akiwa ni mteule wa chama cha ANCCR -MAGEUZI kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo.
Aidha Msimamizi huyo wa Uchaguzi, alimkabidhi fomu ya Uteuzi mgombea huyo, kufuatia Maelekezo ya Fomuya Uteuzi Na. 8B, kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.
Msimamizi Mtambule amemtaka mteule huyo, kusoma maelekezo yaliyotolewa na Tume ya Taifa Ya Uchaguzi, kuheshimu na kufuata taratibu za Uchaguzi kwa kusoma vitini vyenye maelekezo ya taratibu zote za uchaguzi mkuu.
Aidha amemtaka na kufanya kampeni za kistaarabu, muda utakapofika, lengo ni kufanya uchaguzi wa amani, huru na haki kwa maendeleo ya watanzania wote.
Mgombea huyo amefanya kufikisha idadi ya Wagombea kumi na moja, kutoka vyama kumi na moja vya siasa, kuchukua fomu ya Uteuzi, Ubunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi.
*PICHA ZA MATUKIO*
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.