Wakazi wa kijiji cha Lengijave wamesema kuwa wanadhani gharama wanayotumia kutafuta maji ni kubwa kuliko gharama halisi za kulipia maji zinazoendeshwa na Mamlaka za maji zilizopo kisheria.
Wamesema kuwa kijiji chao hakina utaratibu wa kulipia gharama za maji bali huchangishana pale inapotokea changamoto ya uharibifu wa miundombinu ya maji jambo ambalo huwalazimu kutumia muda mrefu na nguvu nyingi ili kupata kiasi kidogo cha maji na kisichotosheleza.
Wameendelea kufafanua kuwa wako tayari kulipia gharama za maji kwa utaratibu utakaowekwa kutokana na adha kubwa ya upatikanaji wa maji wanayoipata wananchi hao licha ya kuwa maji hayo huchotwa bure.
Hayo wameyasema hayo kwenye mkutano kijiji chao baada ya timu ya wataalamu wasimamizi wa mradi wa maji wa 'VIJIJINI VITANO' kutoa mrejesho wa namna maji yatakavyopatikana na jinsi mradi huo utakavyoendeshwa ikiwemo kulipia gharama za maji.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.