• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkakati wa Dkt. Mahera kupandisha ufaulu wazaa matunda

Posted on: November 3rd, 2018

Mikakati ya aliyoiweka Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, ya kupandisha kiwango cha taaluma na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi, imeanza kuzaa matunda mara baada ya wanafunzi wa darasa la saba kufaulu kwa aslimia 89% mwaka 2018.

Matunda hayo mema, yamejidhihirisha wazi baada ya ongezeko la kiwango cha ufaulu na kufikia asilimia hiyo 89, katika matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la saba, mtihani liofanyika mwezi Septemba mwaka 2018, kwa kujibu wa takwimu za matokeo, yalivyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani 'NECTA'.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, ofisini kwake, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, amepata fursa ya kuelezea sababu zilizopelekea kupanda kwa kiwango cha taaluma na ufaulu kwa shuleni,  ni juhudi kubwa za zilizofanyika katika utekelezaji wa mpango mkakati waliojiweke, juhudi ambazo zimewezesha ongezeko kubwa la ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa mwaka huu.

Mkurugenzi huyo, ametaja kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa darasa mwaka 2018, kuwa kimepanda kutoka asilimia 71% ya mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 89%, na kuifanya halmashauri hiyo, kushika nafasi ya 21 kitaifa kati ya halmashauri 185 za Tanzania kutoka nafasi ya 97 ya mwaka 2017, huku ikishika nafasi ya 2 kati ya halmashauri 7 za mkoa wa Arusha kutoka nafasi ya 4 mwaka jana.

Aidha Dkt. Mahera amethibitisha kuwa, ufaulu huo wa wanafunzi unaendelea kuimarika na kupanda kila mwaka ukilinganishwa na miaka mitatu ya nyuma, kutokana na mipango na mikakati mizuri aliyoiwekezwa, kwenye sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa walimu, wanafunzi pamoja na wazazi, huku kukiwa na ufuatiliaji na usimamizi ulio thabiti.

Dkt. Mahera, ameitaja siri kubwa iliyopelekea halmashauri hiyo kupata mafanikio hayo ni kujituma kila mmoja kwa nafasi yake, pamoja na utekelezaji thabiti wa mipango mikakati inayoenda sambamba na kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana kama timu kwa sekta zote zinazohusika na masuala ya elimu

"Nilipofika hapa ufaulu ulikua chini, na walimu walikuwa wamekata tamaaa, lakini nilijitahidi kukaa na kuzungumza nao, kutatua changamoto ndogondogo zilizokuwa zikiwakabili, na kubwa zaidi ilikuwa ni kuwatia moyo, kwa kuwa niliamini kazi kubwa ya kupandisha ufaulu, inafanywa na walimu hivyo walimu wakiwa demoralized, ufaulu haupo, lakini walimu wakijituma kwa moyo lazima wanafunzi watafanya vizuri katika mitihani yao, na ndicho kilichotoke". alieleza Dkt.Mahera.

Ameongeza kuwa sababu nyingine iliyopelekea halmashauri ya Arusha kupata mafanikio hayo makubwa, ni ushirikiano mzuri, uliopo baina ya uongozi wa halmashauri kuanzia ngazi ya wilaya, kata, kijiji mpaka ngazi ya uongozi wa shule pamoja na walimu wenyewe.

Dkt. Mahera amefafanua kuwa, mkakati huo wa kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi haupo kwenye elimu ya msingi pekee bali halmashauri pia imeweka mkakati wa kufuta alama sifuri kwa wanafunzi wa kidato cha nne, kwa kuhakikisha kila mwanafunzi anapata walau 'D' nne katika mitihanj yake, na kuongeza kuwa mkakati huo ulileta matokeo mazuri kwa mwaka 2017, halmashauri ilishika nafasi ya 31 kitaifa kutoka nafasi ya 79 mwaka 2016 na kuwa na ufaulu wa 84.21% huku ikifanikiwa kupunguza idadi ya wanafunzi waliopata alama sifuri  kutoka 1,477 mpaka kufika wanafunzi 608 tu.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amethibitisha, halmashauri hiyo kuendelea kupata matokeo mazuri zaidi kwa kuendelea kushirikiana na Idara ya Elimu kufanya kazi kama timu huku akiwa na jukumu kubwa la kuwahimiza walimu kutekeleza majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kufundisha kwa bidii kwa kufuata miongozo pamoja na viwango vya upimaji wanafunzi  vilivyowekwa na Udhibiti Ubora wa Elimu.

Licha ya kupata matokeo mazuri yaliyowezasha halmashauri ya Arusha kushika nafasi ya 21 kitaifa, Mkurugenzi huyo amezitaja changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na ukosefu wa nyumba za walimu hasa kwenye maeneo ya vijijini jambo linalosababisha shule hizo kuwa na upungufu wa walimu pamoja na baadhi ya wanafunzi kushindwa kupata chakula cha mchana wawapo shuleni, kutokana na mwamko hafifu wa wazazi kuchangia chakula hicho.

Halmashauri ya Arusha ina jumla ya shule za msingi 138 kati ya hizo shule 46 ni za binafsi na shule 92 zinamilikiwa na serikali huku kukiwa na ongezeko kubwa la uandikishwaji wanafunzi kwa shule za serikali, kwa madarasa ya awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza, hii ni kutokana na serikali kutekeleza sera ya elimu bila malipo jambo linalosababisha upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa pamoja na madawati.

Mkurugenzi Mahera anawataka wadau wote wa maendeleo kujitokeza, kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa kuchangia ujenzi wa vyumba vya  madarasa kwa shule za sekondari, ili wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza waweze kupata mahali pa kusomea pamoja na kuwa na mazingira rafiki ya kujifunzia.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.