Mitihani hii ya muhula wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2028, kwa shule za sekaondari mkoa wa Arusha inatarajia kuanza kufanyika, kuanzia tarehe 17-24/05/2018 kwa shule zote za mkoa huo.
Akizungumza na mwandishi wetu, ofisini kwake leo Afisa Elimu Taaluma halmashauri ya Arusha, mwalimu John Charles amesema kuwa, utaratibu huu mpya umeanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha mhe. Mrisho Gambo, maalum kwa lengo la kuboresha na kuinua kiwango cha taaluma kwa wanafunzi katika shule za sekondari za mkoa wa Arusha.
Afisa Elimu Charles amefafanua kuwa mitihani hii ya muhula, itafanyika kimkoa tofauti na utaratibu wa awali uliokuwa umezoeleka, wa mitihani hiyo kutungwa na walimu wa masomo husika ndani ya shule zao.
Ameongeza kuwa mitihani imetungwa pamoja na itasahihishwa pamoja ili kuwapima wanafunzi yale waliyofundishwa kulingana na mitaala ya masomo husika.
" Mada za masomo zinafanana kulingana na madarasa husika, maazimio ya kazi ya walimu yanafuata mtaala mmoja, hivyo upimaji huu utatoa picha halisi ya namna wanafunzi wanafundishwa, na ufundishaji wa walimu, mitihani ni ilele tofauti ni watungaji tu" amesema Afisa Elimu huyo.
Aidha amesema kuwa mitihani hii licha ya kuwapima wanafunzi, itapima pia malengo ya ufundishaji kupitia mitaala kama yanafikiwa, sambamba na kufanya tathmini ya ufundishaji kwa kulinganisha na mpango kazi wa mwalimu.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewahi kunukuliwa akisema kuwa, tafiti zinaonyesha wanafunzi wanafanya vibaya mitihani ya kitaifa kutokana na baadhi ya walimu kutokufundisha na kumaliza mada za masomo kulingana na mitaala.
" Wanafunzi wanaonekana kufanya vizuri sana kwenye mitihani ya ndani, laikini inatokana na mwalimu anafundisha mada anazotaka, anatunga mtihani kwa mada chache alizofundisha, wanafunzi wanafaulu, tatizo ikija mitihani ya kitaifa wanafunzi hawafanyi vizuri, kutokana na watungaji wa kitaifa kutunga mitihani kwa kuzingatia mada zote za darasa husika" alinukuliwa mkuu wa mkoa Gambo.
Hata hiyo mkuu wa mkoa Gambo alisema kuwa kupitia mitihani hii ya pamoja itatoa picha halisi ya ufundishaji wa walimu na uelewa wa wanafunzi, kupitia mada za mitaala ya masomo husika pamoja na maazimio ya kazi ya walimu kwa muda husika.
Hata hivyo Afisa Elimu Charlesa amethibitisha kuwa mitihani hii ya muhula itawahusisha wanafunzi wa kidato cha I , II,III na V na jumla ya shule 54 za sekondari halmashauri ya Arusha zitafanya mitihani hiyo na kuongeza kuwa, tayari maandalizi yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 90%.
Uongozi wa halmashauri ya Arusha, unawatakiwa wanafunzi wote kila la heri katika mitihani yao.
!!!!!...... TUNATEKELEZA.....!!!!!!!!!!!!!
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.