Na. Elinipa Lupembe.
Halmashauri ya Arusha inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendelei katika kata zote 27, kwa lengo la kuhakikisha huduma za jamii zinapatika kwa urahisi na kwa uwiano sawa kwenye maeneo ya miji na vijiji.
Shughuli zote hizo za Maendeleo zinatekelezwa kwa usimamizi wa Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera kwa kushirikiana na watumishi wa ngazi na sekta zote, viongozi wa ngazi zote, kupitia mipango kabambe inayowekwa na Baraza la Waheshimiwa Madiwani.
Dkt. Mahera amefafanua kuwa, halmashauri ya Arusha, imejikita kuelekeza nguvu katika kutekeleza miradi kisekta huku vipaumbele vikiwa kwenye sekta ya Elimu, Afya, Maji, Mazingira na Usafishaji, Kilimo, Mifugo, Ardhi na Marndeleo ya Jamii.
Kwa mwaka wa fedha 2017/2018-2018/2019, Halmashauri inaendelea kutekeleza miradi mipya, miradi ya nje ya bajeti, pamoja na miradi bakaa inayoendelea kutoka mwaka wa fedha uliopita 2015/2016 na mwaka wa fedha 2016/2017.
Mkurugenzi Mahera ameongeza kuwa, halmashauri inatekeleza miradi yake kwa kuzingatia zaidi ushirikishwaji wa wananchi na wadau wa maendeleo ndani na nje ya Tanzania, makampuni, na ASAS za kiraia.
Halmashauri pia inahakikisha miradi hiyo inazingatia weledi ikiwemo usimamizi thabiti wa matumizi ya fedha na utekelezaji unaozingatia thamani halisi ya fedha kwa kulinganisha na ubora wa mradi.
Ameitaja miradi inayotekelezwa ni pamoja na miradi ya Ujenzi na Ukarabati wa Vyumba vya Madarasa, Nyumba za walimu, Bwalo, hosteli pamoja na vyoo vya wanafunzi katika shule za Msingi na Sekondari, Ujenzi na Ukarabati wa Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali pamoja na ujenzi wa nyumba za wahudumu wa Afya ikiwemo madaktari na wauguzi, Ujenzi na Ukarabari wa miundombinu ya barabara pamoja na vivuko, madaraja na mitaro ya kupitisha maji kwenye kingo za barabara.
Aidha Dkt, Mahera amewashukuru na kuwapongeza wananchi wote wa halmashauri ya Arusha kwa ujumla wao, watalamu wa halmashauri kisekta, viongozi wa ngazi zote, wadau wote wa maendeleo kwa mapenzi mema yanayowawezesha kujitoa kwa hali mali kuhakikisha wananchi wote wa halmashauri ya Arusha wanapata Maendeleo na kuwataka wadau wengine wa ndani na nje kujitokeza kuwekeza ndani ya halmashauri hiyo.
Bonyeza link hiyo kona taarifa za miradi katika picha
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.