Na. Elinipa Lupembe.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido, Mheshimiwa Sabore Kennedy Molloimet, amechakuliwa kuwa Mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Arusha, kwenye mkutano wa ALAT Mkoa, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa halmashauri ya Arusha.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Makamu Mwenyekiti, ALAT mkoa wa Arusha na Meya wa Jiji la Arusha, Mheshimiwa Kalist Lazaro, amesema kuwa, uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa kanuni ya za Kudumu za Mikutano ya Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya za mwaka 2009, kifungu cha 42, 43 na 44, hivyo amemtangaza Mwenyekiti halmashauri ya Longido, mheshimiwa Sabore Molloimet kuwa Mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Arusha bada ya kupata kura za ndio zaidi ya nusu.
Amefafanua kuwa mheshimiwa Molloimet, amepata kura 21 za ndio, kati wapiga kura 22 huku kura moja ikiharibika na kumpa dhamana ya kuwa Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Arusha mpaka mwaka 2020.
Naye Mwenyekiti mpya wa ALAT mkoa wa Arusha, mheshimiwa Molloimet licha ya kushukuru wajumbe kumpa dhamana ya kushika nafasi hiyo na kuwaomba wajumbe hao, kushirikiana kwa pamoja na kuweka tofauti zao za kiitikadi kwa maslahi mapana ya wananchi waliowachagua na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mheshimiwa Mwenyekiti huyo, ameahidi kutumia uwezo alionao, kusimamia nafasi hiyo kwa haki na kuwataka wajumbe kutimiza wajibu wao pamoja na kuheshimu makubaliano na kusimamia utekelezaji wake.
"Nashukuru kwa kunipa nafasi hii na uwezo ninao, naahidi kuutumia kwa kutenda haki, na zaidi tutumie nafasi zetu kuwahudumia wananchi kwa maslahi ya watanzania"amesema Mwenyekiti huyo.
Awali Mwenyekiti wa ALAT mkoa, mheshimiwa Sabole Molloimete, amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Mheshimiwa Jubilete Mnyenye, aliyepoteza sifa za kuwa Mwenyekiti wa Jumuia hiyo.
Mwenyekiti mpya wa ALAT mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Sabore Molloimet (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa mkutano huo, mara baada ya kuchaguliwa kuiongoza Jumuia hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.