Na. Elinipa Lupembe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Arumeru, kuondoa hofu, kwani Serikali ya awamu hii, imejipanga kutatatua kero na changamoto zinazowakabili, badala yake kufanyakazi kwa bidii kwa amani na utulivu ili kuleta maendeleo ya nchi yao.
Mheshimiwa Rais amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kikatiti, Wilayani Arumeru mara baada ya kupokelewa na wananchi wa wilaya hiyo, tayari kwa kuanza ziara yake ya kikazi mkoani Arusha, akitokea Mkoani Kilimanjarao.
Hata hivyo mheshimwa Rais imezitaja changamoto hizo ikiwa ni pamoja na miundombinu ya barabara, Maji na huduma za Afya, na kuahidi kuwa serikali ya awamu ya sita imeweka kipaumbele katika kuzifanyiakazi changamoto zinazowakabili wananchi.
Akiwa wilayani Arumeru Mheshimiwa Rais ametoa fedha kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha miundombinu ya zahanati ya Kikatiti, na kusisitiza usimamizi thabiti wa matumizi ya fedha hizo, ili kituo kikamilike kwa haraka kiweze kuwahudumia wananchi.
"Hiyo pesa ni ya moto hailiki, hiyo pesa ni ya moto haitalika, imetolewa kwa zahanati kwa ajili ya wananchi, tunamkakati wa kujenga vituo vya afya zaidi ya 200 nchi nzima kupitia fedha zinazotokana na tozo za miamala" amesisitiza mheshimiwa Rais.
Awali, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, ziara ambayo atatembelea mradi mkubwa wa Maji wa Jiji la Arusha na kukagua tanki kubwa la maji 'sub station' eneo la Chekereni kijiji cha Mlangarini, atazindua hospitali ya Jiji la Arusha na baadaye kuzungumza na wananchi katika uwanja cha Sheikh Amri Abeid.
Katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Arusha, Mheshimiwa Rais atakwenda wilayani Longido na kuzindua kiwanda cha Nyama, kuzindua wa mradi wa Maji Longido na baadaye kufafanya Mkutano wa hadhara eneo la Stendi mpya Longido.
Mkoa wa Arusha
#kaziinaendelea✍✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.