Matengenezo ya barabara ya Sanawari- Olturoto - Oldonyosapuk, yanaendelea vizuri baada ya kukwama kwa muda, kutokana na zoezi la kuhamishs mabomba ya maji yaliyokuwa yametandazwa kwenye barabara hiyo.
Mambomba hayo, yanayopeleka maji Jiji la Arusha na kumilikiwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira AUWSA na kusababisha mradi huo kushindwa kukamilika kwa wakati na kushindwa kukamilisha mita za barabara zilizopangwa kutengenezwa kutokana na kiasi cha fedha kutumika kuhamisha mabomba hayo.
Akizungumza na mwandishi wetu alipotembelea barabara hiyo, Meneja wa Wakala wa barabara mijini na vijijini 'TARURA', Mhandisi Sangeti Kilusu, amesema kuwa kwa sasa matengenezo ya barabara hiyo yanaendelea vema, baada ya kukamilika zoezi la kuhamisha mabomba yaliyokuwa yametandazwa barabarani.
Kilusu ameongeza kuwa, zoezi la kuhamisha mambomba hayo licha ya kukwamisha kwa muda shughuli za matengenezo pia limesababisha kushindwa kutengeneza barabara hiyo kwa muda uliyopangwa, na badala yake kumalizika mwezi wa Mei badala ya mwezi Machi, 2018.
Aidha mhandisi Kilusu amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa, zoezi la uhamishaji wa mabomba hayo limeongeza gharama za fedha ambazo hazikuwepo kwenye mpango ya ujenzi 'BOQ' wakati ukiandaliwa.
"Imelazimika kupunguza ujenzi wa barabara kwa urefu wa mita 300 kutoka mita 1000 zilizopangwa kutengenezwa, na badala yake barabara hiyo kutengenezwa urefu wa mita 700, kutokana na kulazimika kutumia fedha za mita 300 kuhamisha mabomba ya maji" amesema Mhandisi Kilusu.
Barabara ya Sanawari-Timbolo inajengwa kwa kiwango cha lami, kwa urefu wa mita 700 kwa gharama ya shilingi milioni 369 na inategemea kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei, 2018.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.