Na. Elinipa Lupembe.
#Amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kuishi kwa upendo kama familia moja na kufanya kazi kama timu, ili kufanya mazingira ya kazi kuwa rafiki.
#Watumishi kuheshimiana na kuthaminiana katika enelo la kazi ni nguzo ya utendaji uliotukuka, kila mtumishi anathamani yake katika kazi, kuanzia yule wa ngazi ya chini kabisa, kwa pamoja tunawajibu wa kuwatumikia wananchi bila kutharauliana.
#Watumishi kufanyakazi kwa weledi, kwa kufuata miongozo, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma kwa kuwahudumia wananchi ili kuleta maendeleo ya halmashauri na Taifa kwa ujumla.
#Serikali imewaamini watumishi na kuwapa dhamana ya kulitumikia taifa hili, tumieni taaluma zenu kufanyakazi za kuwahudumia wananchi kwa upendo bila ubaguzi, toeni huduma zinazostahili na kwa wakati.
#Kuwahi kazini ni jambo la muhimu sana, kubwa zaidi ni kutumia muda wa kazi kufanyakazi za serikali, muda wa kutoka kazini ni pale mtumishi anapokuwa amemaliza au kukamilisha kazi zake za siku.
#Kila mtumishi anafahamu majukumu yake, fanyeni kazi kwa kujiamini bila woga, sitapenda uzembe kazini, wala kusukumana kufanyakazi, na sitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wazembe lakini sitapenda tufikie huko.
#Serikali ya awamu ya tano imelenga kuto huduma kwa wananchi kwa kuwafikishia huduma hizo katika maeneo yao, tusikae ofisini, tokeni kuwahudumia wananchi wetu hasa wale wa hali ya chini, Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli anaridhishwa na utumishi wenye tija, wenye kuwahudumia wananchi, hivyo tushirikiane kuunga mkono juhudi hizo za Serikali iliyoko madarakani.
#Tutambue kuwa sisi kuwepo Arusha DC ni neema ya kipekee ya Mungu hivyo tupendane, tuheshimiane, tuthaminiani wakubwa kwa wadogo, ili tuweze kuwatumikia wananchi kwa amani na pendo.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Alvera Ndabagoye akiwasili katika ofisi za makao makuu ya halmashauri hiyo.
Kaimu Mkurugenzi, halmashauri ya Arusha, Anastazia Tutuba akimkaribisha mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, Alvera Ndabagoye alipowasili katika ofisi za makao makuu ya halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Alvera Ndabagoye akisaini kitabu cha wageni katika ofisi yake mpya, mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za makao makuu ya halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Alvera Ndabagoye akizungumza ma Timu ya Menejimenti (CMT) Wakuu wa Idara na Vitengo kwenye Ofisi yake mpya.
Watumishi wa halmashauri ya Arusha, wakimsikiliza mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Alvera Ndabagoye, kwenye ukumbi wa mikutano wa shule ya msingi ya Green Acreas
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.