Madiwani watatu kutoka kata tatu za hamashauri ya Arusha, wameapishwa leo, kutumikia nafasi hizo, wakati wa Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, amewataja madiwani hao kuwa ni Mheshimiwa Raymond Lairumbe wa kata ya Oldonyosam, mheshimiwa Lembris Mollel wa kata ya Ilboro na mheshimiwa Godfray Mashele wa kata ya Mlangarini.
Madiwani hao, wameapishwa baada ya kupita bila kupingwa, kufuatia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kutangaza uchaguzi mara baada ya Madiwani hao, kukihama kilichokuwa chama chao, Chama cha Demokrasia na Maendeleo - (CHADEMA) na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) mapema mwezi ulipita.
Aidha Madiwani hao, Waliapishwa na Waakili Patricia Kisinda, baada ya Mwanasheria, wa halmashauri ya Arusha, Eliasifiwe Kileo kuelezea, uhalali wa Madiwani hao kuapishwa na kufafanua kuwa, Madiwani hao wanaapishwa kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa sura ya 292.
Hata hivyo kwa mujibu wa Kanuni ya 56 kifungu kidogo cha pili ya Tume ya Taifa ya uchaguzi, Msimamizi mkuu wa Uchaguzi, ngazi ya Halmashauri na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera amewakabidhi vyeti vya udiwani, madiwani hao watatu.
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KUAPISHWA MADIWANI
Mheshimiwa Lembris Mollel Diwani wa kata ya Ilboru, akila kiapo wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani, kwenye ukumbi wa Mikutano, halmashauri ya Arusha.
Mheshimiwa Raymond Lairumbe, Diwani wa kata ya Oldonyosambu, akila kiapo mara baada ya kupita bila kupingwa kwenye kata yake, amekula kiapo hicho, wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani, kwenye ukumbi wa Mikutano, halmashauri ya Arusha.
Mheshimiwa Godfray Mashele, Diwani wa kata ya Mlangarini, akila kiapo mara baada ya kupita bila kupingwa, Diwani huyo ameapishwa wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani, kwenye ukumbi wa Mikutano, halmashauri ya Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Dkt, Wilson Mahera akimkabidhi cheti cha Udiwani, Mheshimiwa Raymond Lairumbe, Diwani wa kata ya Oldonyosambu, mara baada ya kuapishwa wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani, kwenye ukumbi wa Mikutano, halmashauri ya Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Dkt, Wilson Mahera akimkabidhi cheti cha Udiwani, Mheshimiwa Godfray Mashele, Diwani wa kata ya Mlangarini, mara baada ya kuapishwa wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani, kwenye ukumbi wa Mikutano, halmashauri ya Arusha.
Mheshimiwa Lembris Mollel Diwani wa kata ya Ilboru, akionyesha cheti cha udiwani mara baada ya kuapishwa, wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani, kwenye ukumbi wa Mikutano, halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.