Madiwani watatu wa CHADEMA watimkia CCM.
Madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, wamekihama chama hicho na kuhamia Chama cha Mapinduzi -CCM, kufuatia kile wanachodai ni kuridhishwa na utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na chama tawala cha CCM.
Madiwani hao ni pamoja na Mheshimiwa Losieku Kulisu wa kata ya Lemanyata, Mheshimiwa Ojung Salekwa, diwani kata ya Laroi na Mheshimiwa Loth Mungaya, diwani kata ya Ilkiding'a.
Madiwani hao wamesema kuwa wameridhishwa na kasi ya Maendeleo inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano na kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kwa moyo wake wa uzalendo wa kuleta maendeleo kwa watanzania.
Wamethubitisha kuwa, kwa kipindi cha muda mfupi wa awamu ya tano, Serikali ya Tanzania imepig hatua kubwa ya maendeleo kwenye sekta za Elimu, Afya, Maji, miundombinu ya barabara pamoja na usafiri wa anga hali inayoonyesha dira ya kufikua uchumi wa kati ifikapo 2025 na kuiondoa Tanzania kwenye nchi masikini duniani.
Akizungumza wakati wa kuwakabidhi kadi za CCM madiwani hao, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arumeru, Simon OleSaning'o amewapongeza madiwani hao kwa kufanya uamuzi makini wa kurudi nyumbani na kuahidi kuwapa ushirikiano kwa lengo la kuwatumikia watanzania wanaohitaji maendeleo kwa sasa.
Mwenyekiti Ole Saning'o amewasisitiza Madiwani hao, kufanyakazi kwa bidii na kutekeleza Ilani ya CCM yenye lengo la kuwatumikia wananchi pamoja na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Magufuli aliyejitolea kuwahudumia wananchi wanyonge kwa maendeleo ya Serikali yao ya Tanzania.
Mpaka sasa, jumla ya Madiwani 11 walichaguliwa kupitia CHADEMA, kwenye uchaguzi mkuu 2015, wameshakihama chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi na kufanya CCM kuwa na jumla ya madiwa 16 katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Arusha, katika jimbo la Arumeru Magharibi.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arumeru, Simon Ole Saning'o akimkabidhi Kadi ya CCM, diwani wa kata ya Laroi, Mheshimiwa Ojung'u Salekwa, mara baada ya kukihama chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kuhamia Chama cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arumeru, Simon Ole Saning'o akimkabidhi Kadi ya CCM, Diwani wa kata ya Ilkiding'a Mheshimiwa Loth Mungaya, mara baada ya kukihama chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kuhamia Chama cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arumeru, Simon Ole Saning'o akimkabidhi Kadi ya CCM, Diwani wa kata ya Lemanyata Mheshimiwa Losieku Kilusu mara baada ya kukihama chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kuhamia Chama cha Mapinduzi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.