Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta uliosababishwa na maji yaliyotokana na mvua iliyonyesha usiku wa kuamakia leo katika eneo la Mangurueni kitongoji cha Ilkiurei kata ya Kiranyi halmashauri ya Arusha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha kamishna Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja mtu aliyefariki ametambulika kwa jina la Fatiki Kingazi mwanaume anaekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25-30 mkazi wa Unga Ltd Jijini Arusha ambaye alikwenda kumtembelea ndugu yake bi. Rukia Hassan ndipo mauti yalipomkuta.
Katika tukio hilo jumla ya familia 30 hazina mahali pa kuishi kutokana na nyba zao kujaa maji.
Hata hiyo Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Arusha ndugu Charles Pallangyo amefungua kambi katika shule ya msingi Ilkiurei kwa ajili ya kuwahifadhi watu wa familia 30 amabazo hazina mahali pa kuishi na kuammuru nyumba hizo kufungwa kwa muda mpaka utakapopatikana ufumbuzi wa tatizo hilo la kujaa maji.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.