KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA KINYWA NA MENO DUNIANI TAREHE 20.03.2020.
Halmashauri ya Arusha kupitia watalamu wake wa Idara ya Afya, itatoa huduma mbalimbali za afya katika Zahanati ya Esther eneo la Ngaramtoni kuanzia tarehe 16 - 20/03/2020.
HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA NI PAMOJA NA:
1.Upimaji wa Afya ya kinywa na meno.
2. Upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza (sukari, BP nk)
3. Huduma ya uzazi wa mpango na Afya ya Uzazi
4. Upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi
5. Huduma ya afya ya akili
Huduma hizo zitatolewa Bure kwa siku zote 5 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
Kila mwananchi anatakiwa kufika kupata huduma hizo.
Ukisikia Tangazo hili mwambie na jirani yako.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.