Na. Elinipa Lupembe.
Shirika lisilo la kiseriksli la Ace Africa limetoa msaada wa komputa tano na lota mbili kwenye kituo cha afya cha Olkokola kata ya Lemanyata, halmashauri ya Arusha.
Vifaa hivyo ya kisasa vimetolewa, kwa lengo la kuboresha utoaji na upatikanaji wa huduma bora za afya kupitia miundombinu wezeshi inayorahishisha uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu sahihi za wagonjwa na kituo kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mratibu wa mradi wa shirika la Ace Africa, John Emmanuel amesema kuwa, wamekabidhi vifaa hivyo kwa ajili ya kuboresha uhifadhi na utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa kwa njia ya mtandao, kwa kutumia Komputa tano na lota mbili zenye thamani ya shilingi milioni 5.4.
Mratibu huyo, ameongeza kuwa shirika hilo linaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano, katika kuboresha miundo mbinu ya afya, na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za magonjwa ya kawaida katika maeneo yao, pindi wanapougua.
"Komputa hizi zinatumia mtandao na server itakuwa Hospital ya Wilaya Olturumet, hivyo itawarahisishia wauguzi kazi ya kusafiri kupeleka taarifa makao makuu kwa kutumia makaratasi, taarifa zitatumwa kupitia mfumo na ukiserve kumbukumbu yoyote, tayari mtu wa makao makuu atazioa taarifa hizo "amesisitiza John
Naye Mganga Mkuu halmashauri ya Arusha Dkt. Petro Mboya amelishukuru shirika la Ace Africa kwa kutoa vifaa hivyo muhimu, vitakavyorahisisha utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa kwa njia ya mtandao na kuwataka wahudumu wa kituo hicho kutumia komputa hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa na zaidi kuvitunza vifaa hivyo.
Mganga mkuu huyo, amewataka pia wauguzi hao kufanyakazi ya kuhudumia wagonjwa kwa weledi, kwa kuwa sasa kazi ya kutunza na kutuma kumbukumbu imepungua, hivyo ni vema kutumia muda huo kuhudumia wagonjwa.
"Kazi ya kusafiri kupeleka taarifa makao makuu haitakuwepo sasa, mtatuma taarifa hizo kupitia mtandao, hivyo tumieni muda huo kuhudumia wagonjwa kwa kutoa huduma iliyo bora" amesema Daktari Mboya
Olais Kiken mkazi wa Olkokola amethibitisha kuridhishwa na vifaa hivyo kwenye kituo chao cha afya na kuongeza kuwa, anaamini sasa historia ya mgonjwa itahifadhiwa na hata akipoteza cheti hakutakuwa na kazi ya kuanza upya kujieleza.
" Huwa tunapata shida pale mgonjwa anapopoteza cheti, inamlazimu kuanza upya matibabu, lakini tumeambiwa mtandao unatunza kumbukumbu zote za mgojwa" amesema mzee Kiken
Hata hivyo wauguzi wa kituo cha Afya cha Olkokola, licha ya kulishukuru shirika la AceAfrica kwa msaada huo wameahidi kuvitunza na kufanyia kazi vifaa hivyo ambavyo kimsingi vitawarahisishia kazi hasa katika utunzaji wa kumbukumbu muhimu za kituo na wagonjwa pia.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.