Wauguzi halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru wametakiwa kuacha kufanyakazi kwa mazoea na badala yake kufanya kazi wa weledi na zaidi kwa kuzingatia maadili ya fani ya Uuguzi na yale ya Utumishi wa Umma.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri hiyo Dkt.Wilson Mahera wakati akifungua kikao kazi cha siku moja kilichokutanisha karibu Wauguzi wote wa halmashauri hiyo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Halmashauri ya Arusha.
Dkt. Mahera amesema kuwa fani ya Uuguzi ni nyeti sana inayohitaji umakini, uadilifu, huruma na upendo kwa wagonjwa anaohitaji huduma wakati wakiwa katika hali isiyo ya kawaida.
Ameongeza kuwa Serikali imewaamini Wauguzi na kuwapa dhamana ya kuhudumia wagonjwa hivyo tumieni taaluma zenu kuhudumia wagonjwa bila kujali hali zao ili kujenga imani kwa wagonjwa mnaowahudumia.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.