Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt (MST) George Mkuchika ametoa Kauli ya Serikali Bungeni leo, kuhusu watumishi walioondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mshahara kwa kukosa sifa ya cheti cha kufaulu mtihani wa elimu ya kidato cha nne.
Mhe. Mkuchika ametoa kauli hiyo ya serikali na kufafanua mambo yafuatayo:-
# Watumishi wote ambao wana Ajira za Kudumu au Ajira za mikataba (Kwa Watendaji wa Vijiji na Mitaa) au ajira za# Watumishi wote ambao wana Ajira za Kudumu au Ajira za mikataba (Kwa Watendaji wa Vijiji na Mitaa) au ajira za muda (Employment on Temporary Terms) ambao walikuwa kazini kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 ulipoanza kutumika Waraka wa utumishi( Establishment Circular) Na. 1 wa mwaka 2004, Warejeshwe kazini Mara moja, walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu wa sheria.
# Watumishi wa Umma Elfu Moja mia tatu sabini (1370) waliolegezewa masharti ya sifa za muundo kupitia barua ya Katibu Mkuu Utumishi yenye Kumb. Na. CCB.271/431/01/P/13 ya tarehe 30 Juni, 2011, warejeshwe kazini mara moja, walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu wa sheria.
# Uamuzi huo hautawahusu Watumishi waliowasilisha vyeti vya kughushi katika kumbukumbu za ajira yao.
# Watumishi walioajiriwa baada ya Mei 20, 2004 wakiwa hawana sifa za kufaulu mtihani wa kidato cha nne kwa kuwa walijipatia ajira kinyume cha maelezo ya Serikali.
# Aidha Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi wote walioshiriki kuwaajiri Watumishi wasiokuwa na sifa ya kufaulu mtihani wa kidato cha nne katika Utumishi wa Umma baada ya Mei 20, 2004 watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.
# Watendaji Wakuu na Maafisa wote wanaosimamia zoezi hili kwa kuondoa au kuharibu kumbukumbu za Watumishi ili haki isitendeke, watachukuliwa hatua za kinidhamu na za kijinai ikibidi.
*Imeandaliwa na Idara ya Habari - MAELEZO.*
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.