Na. Elinipa Lupembe.
Wasanii wa vichekesho mkoa wa Arusha, wameanza kampeni ya kuchangia damu kwa hiari, ikiwa ni Kampeni ya kudumu ya Changia damu kwa hiari, inayokwenda kwa jina la 'Changia Damu na Katarina wa Karatu', kampeni iliyoanza rasmi mwisho ni mwa mwaka 2020, ikiwa na lengo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiari.
Wakizungumza wakati wa zoezi la kuchangia damu, lilifanyika katika zahanati ya Ester, iliyoko eneo la Ngaramtoni, halmashauri ya Arusha, wasanii hao wamesema kuwa, lengo lao kubwa kama wasanii ni kuhamasisha jamii kushiriki kuchangia damu kwa hiari, damu itakayotumika kwenye hospitali ya wilaya ya Arusham hospitali ya Olturumet.
Rose Urio maarufu kama Katarina wa Karatu (Rose Urio) na Mwenyekiti wa Kampeni hiyo, ameweka wazi kuwa wao, licha ya kuwa wanajikita kwenye kuburudisha jamii, wameamua kutumianfursa hiyo kuhamasisha jamii kushiriki uchangiaji wa damu kwa hiari, ilimkuokoa maisha ya watanzania wagonjwa wenye uhitaji wa damu.
"Tumeanza kampeni hii mwezi Novemba 2020, ambapo tunahamasisha uchangiaji wa damu kwa ajili ya hospitali zetu za wilaya, na tunafanya zoezi hili kila baada ya miezi 4, mwezi Novemba tulikuwa eneo la Meru kwa ajili ya hospitali ya Nkoarangara, na leo tuko hapa Ngaramtoni kwa ajaili ya hospitali ya wilaya ya Olturumet, tunashukuru wananchi wamejitokeza na tunaendelea kuaisistiza wqnanchi kujenga tabia ya kuchangia damu kwa hiari" amesema Katarina wa Karatu.
Naye mratibu wa zoezi la uchangiaji damu kwa hiari la Changia Damu na Katarina wa Karatu, na Afisa Mtendaji kata ya Kisongo, John Nkini, amewapongeza wasanii hao kwa kujitoa kwa ajili ya afya na uhai wa watanzania, kwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa damu katika hospitali zetu za wilaya, kwa kufanya hivyo kutaokoa maisha ya wananchi wengi hasa wasio na na kuwataka wasanii wengine kujitokeza kusaidia jamii, kama kurejesha sehemu ya mapato yao kama fadhilamkwa jamii 'corprate social responsibilti CSR'
Afisa Ustawi wa Jamii, halmashauri ya Arsuha, Beatrice Tengi, amesema kuwa, halmashauri imeweka utaratibu wa jamii kushiriki mara kwa mara kuchangia damu kwa hiari, hivyo jamii inatakiwa kutambua umuhimu wa uchangiaji wa damu kwa hiari ili kusaidia wagonjwa wanohitaji damu kwa dharura, na kutaja makundi ya wagonjwa yanayohiyaji damu mara kwa mara ni pamoja na wagonjwa wa kansa, selimundu pamoja na kinamama wajawazito na watoto.
Mratibu wa Maabara, halmashauri ya Arusha, Tatu Galingulwa amesema kuwa, halamshauri ya Arusha inahitaji damu kiasi cha Uniti 110 mpaka 120 kwa mwezi, kwa ajili ay hospitali za wilaya ya Olturumet, Seliani, Kivulininna kituo cha Afya Nduruma.
Aidha Mratibu huyo amehimiza watu kujitokeza kuchangia damu kwa hiari huku akisistiza kwamba, kiafya Mwanaumme ana uwezo wa kuchangia kila baada ya mezi 3 yaani mara 4 kwa mwaka, na mwanamke anauwezo wa kuchangia damu mara tatu kwa mwaka na kila baada ya miezi 4.
Awali Kampeni ya Changia Damu na Katarina wa Karatu, imejumuisha wasanii wa vichekesho Arusha, akiwemo Katarina wa Karatu, Mama Nairo, Masai mmbeya, imefanikiwa kukusanya Uniti 27 za damu, ambazo zitatumika kwenye banki ya halmashauri hospitali ya wilaya ya Olturumet na kugawanywa kwenye hospitali nyingine kwa kadiri ya uhitaji.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.