Kamati ya utekelezaji wa mradi wa TUPANGE PAMOJA na TUWAVUSHE SALAMA, halmashauri ya Arusha, wakipanga mikakati, kwa ajili ya kwenda kutoa Elimu elekezi kwa watoa huduma za afya, kwenye Vituo vya 15 ndani ya halmashauri ya Arusha.
Kamati hiyo yenye watalamu wa afya na fani nyingine zinazohusiana na afya, inakwenda kutoa mafunzo namna bora ya utoaji HUDUMA RAFIKI KWA VIJANA, juu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa vijana, kwenye vituo vya Afya vilivyo kwenye mradi.
Vituo hivyo vya afya ni pamoja na Zahanati ya Moivo, Esoka, Ester, Themi ya simba, Musa, Olkokola, Imbibia, Ng'ires, Olmotony, Oldonyosupuk, Olturumet, Mlangarini, Sambasha, Manyire na Olgilai.
Mradi huo unatekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja kwa ushirikiano wa halmashauri ya Arusha na Shirika la JHPIEGO.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.