Wauguzi Halmashauri ya wilaya ya Arusha wanategemea kufanya maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani itakayofanyika tarehe 12.05.2018 kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Nduruma.
Akizungumza na mwandishi wetu, Muuguzi Mkuu halmashauti ya Arusha, Sista Agusta Komba amesema kuwa maadhimisho hayo yatatanguliwa na shughuli za utoaji huduma za afya 18 zitatolewa bure kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 09.05.28 mpaka siku ya kilele ya tarehe 12.05.2018.
Ameomgeza kuwa kati ya hizo huduma zaidi ya kumi zitahusisha upimaji wa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Saratani shingo ya mlango wa kizazi kwa wanawake, magonjwa ya akili, macho, sukari na shinikizo la damu, Fistula, VVU, kifua kikuu, lishe pamoja na kutoa tiba na ushauri nasaha.
Hata hivyo Sista Komba, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kituo cha Afya Nduruma ili kupata huduma hizo, ambazo zinatolewa bure na kuongeza kuwa kwa siku zote nne watoa huduma watakuwepo kuanzia asubuhi mpaka saa 17:00 jioni.
Niwaombe wananchi wa kata za Bwawani, Mlangarini na Nduruma yenyewe kutumia fursa hii, ambayo ni adimu kwao kutokana na mazingira hali halisi ya upatikanaji wa huduma hii kwenye maeneo hayo". Amesisitiza Sista Komba
Kwa siku hizo huduma zitatolewa kuanzia saa 02:00 asubuhi mpaka saa 12:00jioni.
Huduma zitakazotolewa ni pamoja na:-
1. Uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake.
2.Utoaji wa chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14. 3. Upimaji wa Sukari na shinikizo la damu. 4. Upimaji wa VVU
5. Uchunguzi wa Fistula
6. Uchunguzi wa Kifua Kikuu TB.
7. Uchunguzi wa afya ya akili.
8. Uchunguzi wa macho
9. UChunguzi wa lishe
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.