Na. Elinipa Lupembe
Serikali ya awamu ya tano, imeendelea kuboresha miundombinu ya shule za sekondari kupitia Miradi ya Lipa Kutokana na Matokeo ' Education Payment for Result' (EP4R), kwa kuhakikisha shule za sekondari zinakuwa na maabara kwa ajili ya masomo ya Sayansi.
Lengo hasa la serikali likiwa, ni kuwapa fursa wanafunzi kujifunza kwa nadharia na vitendo, ili kupata watalamu wanaoendana na mabadiliko ya Sayansi na teknolojia, kufuati uchumi wa viwanda nchini na kutekeleza lengo la serikali la kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.
Shule ya sekondari Matevesi ni moja ya shule ndani ya halmashauri ya Arusha, iliyopata neema ya kuwa na miundombinu ya maabara 3 za masomo ya Fizikia, Baiolojia na Kemia kupitia mradi wa EP4R kiasi cha shilingi milioni 25 .
#TUMEAMUA#TUNATEKELEZA#
'HAPA KAZI TUU'
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.