Na. Elinipa Lupembe.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amekabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Kaim Mkurugenzi, ambaye ni Afisa Elimu Msingi wa halmshauri hiyo, Mwl. Hossein Mghewa.
Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ofisi ya mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, ambapo aliyekuwankaim mkurugenzi amemkabishi mkurugenzi huyo, kabrasha lenye taarifa iliyosheheni mpango wa shughuli za utekelzaji wa halamashauri ya Arusha, huku Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Mheshimiwa Ojung'u Salekwa akishuhudia zoezi hilo maalum la makabidhiano.
Hata hivyo Mkurugenzi Msumi, amepokea kijiti hicho cha kuingoza halmshauri ya Arusha kwa kuweka wazi vipaumbele vyake ikiwa pamoja na kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuwapa fursa kushiriki na kufahamu huduma zinazotolewa na halmàshauri pamoja na mambo yanayoendelea katika halmashauri yao.
"Ni haki ya kila mwananchi wa halmashauri ya Arusha, kufahamu huduma zinazotolewa na halmashauri ya pamoja na kupata habari za mambo yanayofanyika kwenye halmashauri yao, kupitia tovuti ya halmashauri na kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, hivyo, habari katika channel hizo zote zinatakiwa kuuhishwa mara kwa mara" ameeleza Mkurugenzi Msumi.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha mheshimiwa Ojung'u Salekwa licha ya kumpongeza mkurugenzi huyo kwa kuteuliwa kuingoza halmashauri ya Arusha, amemuhakikishia kuwa ameipokea halmashauri hiyo ikiwa ni salama yenye watumishi wanaojituma katika kazi, na kumuahidi kushirikiana nae katika kutekeleza mipango na mikakati ya halmashauri kupitia miradi katika sekta zote, iliyo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.
Aidha Mheshimiwa Salekwa hakusita kumpongeza aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mwl. Mgewa kwa kuongoza halmashauri kwa kipindi chote ambacho alikaimishwa ofisi hiyo, kwa kuwa hakuwahi kutetereka.
Naye Afisa Elimu Msingi mwl. Mghewa mara baada ya kukabidhi kijiti hicho, ameishukuru familia yote ya halmashauri ya Arusha, ikiwemo Mwenyekiti wa halmshauri, Baraza la Waheshimiwa Madiwani, timu nzima ya menejimenti, watumishi wote, wadau wa maendeleo pamoja na wananchi wa halmashauri hiyo kwa ushirikiano mkubwa, waliompa katika kipindi chote cha kukaimu kwake, ofisi hiyo ya mkurugenz.
Hata hivyo amewataka kumpa ushirikiano huo huo Mkurugezni Mtendaji aliyeteuliwa na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza halmashauri hiyo.Mkurugenzi Msumi anakuwa Mkurugenzi wa sita kuiongoza halmashauri ya Arusha tangu kuanzishwa kwake Julai 2007, baada ya kugawanywa iliyokuwa halmashauri ya wilaya ya Arumeru na kupata halamsahuri mbili za Arusha na Meru zote zikiwa katika wilaya ya Arumeru
.**TUNAMTAKIA KILA LENYE KHERI MKURUGENZI MSUMI**
ARUSHA DC
KAZI INAENDELEA..✍✍
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi (kushoto) akipokea kabrasha lenye taarifa za halamshauri hiyo kutoka kwa aliyekuwa kaimu mkurugezi Mwl. Hossein Mghewa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Ojung'u Salekwa (kulia) akimkabidhi kabrasha lenye taarifa za halamshauri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.