• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC Kimanta awaonya viongozi wanaowahamasisha wananchi kukataa kulipia huduma za maji

Posted on: April 7th, 2018

           Kaimu mkuu wa wilaya ya Arumeru na Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe, Idd Kimanta amekemea tabia ya baadhi ya  viongozi wa kisiasa kuzuia wananchi kulipia huduma za maji na badala yake kujikita zaidi, kuwaelimisha umuhimu wa kulipia huduma hiyo.        

        Kaimu mkuu huyo wa wilaya  amesema hayo wakati wa akinduzi rasmi  bodi mpya ya Mamlaka ya Maji Ngaramtoni 'NGAUWSA' baada ya wajumbe wake kuteuliwa na waziri mwenye dhamana wa ofisi ya Rais TAMISEMI.    

        Mheshimiwa Kimanta ameeleza kuwa kuna baadhi ya viongozi ambao huwashawishi wananchi kukataa kulipia huduma ya maji kwa madai kuwa, huduma hiyo inagharamiwa na serikali jambo ambalo si la kweli.       

       Amefafanua kuwa, ifike wakati viongozi kuacha siasa kwenye suala la maji na kuwataka viongozi  kuwahamasisha wananchi wao, kujua umuhimu na faida za kulipia huduma za maji na si kuwadanganya na kuwapoteza wakatae kulipia maji. 

       " Nina uzoefu kuna baadhi ya viongozi wanawaambia wananchi wasilipe maji, viongozi, waelezeni wananchi ukweli, huduma ya maji inalipiwa na hakuna maji ya bure! Hivi bomba likiharibika litatengenezwa na nani?"   Amehoji Kimanta.     

          Aidha Kimanta amefafanua kuwa huduma ya maji ni lazima ilipiwe, na ipo kisheria, ili miradi ya maji iweze kujiendesha na wananchi kuwa na uhakika wa kupata huduma hiyo kila siku.      

        Hata hivyo amewataka wananchi kutambua kuwa kazi ya serikali ni kujenga miundo mbinu ya maji na kuhakikisha huduma imewafikia wananchi lakini kuiendeleza miradi hiyo ni jukumu la wananchi kwa kulipia huduma hiyo.  

      "Fedha amabazo wananchi wanalipia maji hutumika kukarabati miundo mbinu ya maji, kulipa wahudumu pamoja na kuongeza uwanda wa upatikanaji wa maji kwa watu wasiokuwa na maji" amesema Kimanta.      

         Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha mheshimiwa Noah Lembris amesisitiza kuwa suala lolote la maendeleo ya wananchi halihitaji siasa, viongozi kwa kushirikiana na wananchi  wanatakiwa kujitoa katika shughuli za maendeleo bila kujali tofauti zao za kiitikadi.  

            Na kuongeza kuwa wanatambua Bodi ya maji ipo kisheria, jambo la muhimu ni kuwapa ushirikiano wajumbe wa bodi hiyo ili kuhakikisha wananchi wa Ngaramtoni wanapata huduma ya maji safi na salama na si vinginevyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DKT. PASCAL KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 19, 2025
  • WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

    June 17, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.