Na. Elinipa Lupembe.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mheshimiwa Jerry Muro amekula kiapo, cha kuanza rasmi kuitumikia nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya, mara baada ya kuteuliwa na mheshiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu huyo wa Wilaya amekula kiapo cha utii, mbele ya mkuu wa mkoa wa Arusha, mhe. Mrisho Gambo, huku akiahidi kutekeleza kwa kasi, Ilani ya Chama cha Mapinduzi - CCM na kuwataka viongozi wa wilaya hiyo kwenda pamoja na kuwaonya, wasiotaka kutekeleza Ilani hiyo, kuachia ngazi mapema.
"Nimekuja Arumeru kuwatumikia wananchi, kama Ilani ya uchaguzi ya CCM inavyoelekeza nipo tayari kuitekeleza, kwa yoyote asiyetaka kutekeleza ilani ya CCM aondoke kabla sijaingia ofisini" amesisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.
Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya za Arumeru na Longido, mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amewataka viongozi hao kutumia busara na hekima, wakati wa kutoa maamuzi, yanayohusiana na changamoto zinazoikabili jamii ya watanzania, kwenye maeneo yao ya kazi.
Mhe. Gambo ametaja changamoto kubwa inayoikabili wilaya ya Arumeru ni migogoro ya ardhi, na kumtaka mkuu huyo wa Wilaya, kutatua changamoto hiyo kwa kuzingatia miongozo, kanuni na sheria za serikali huku akiongozwa na hekima na busara.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Longido, mhe. Frank Mwaisumbe amemshukuru rais kwa kumteua na kuahidi kuchapa kazi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.