Na Elinipa Lupembe.
Wadau mbalimbali wa Elimu nchini, wameendelea kujitokeza, siku hadi siku, kuchangia sekta ya Elimu, katika Halmashauri ya Arusha, lengo likiwa ni kuboresha na kuweka mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia, sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayo toa Elimu bila malipo.
Chuo kikuu cha Mzumbe, kimeingia makubaliano na wananchi wa kijiji cha Kiseriani kata ya Mlangarini Halmashauri ya Arusha, kuanzisha ujenzi wa mpya ya sekondari Kiseriani kwa kujenga vyumba vinne vya madarasa, ofisi za walimu, pamoja na vyoo.
Miundombinu hiyo ya Elimu, imegharimu kiasi cha shilingi milioni 150, fedha zilizotolewa na chuo kikuu cha Mzumbe, zikiwa ni fidia ya shamba lililotolewa na kijiji cha kiseriani kwa chuo kikuu hicho.
Afisa Elimu sekondari Halmashauri ya Arusha mwalimu Medad Lupenza, amepongeza uongozi wa chuo kikuu cha Mzumbe na kijiji cha kiseriani, kwa kufanya makubaliano hayo muhimu kwa sekta ya elimu, makubaliano ambayo yameleta mapinduzi ya kielimu katika eneo ambalo, hapo awali halikuwahi kuwa na na shule ya sekondari.
Amethibitisha kuwa, watoto wa kijiji cha Kiseriani, walilazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 10 kufata shule ya sekondari iliyo kijiji cha Mlangarini, umbao ambao ulikwamisha maendeleo ya kitaaluma kwa watoto wengi, na kuongeza kuwa, uwepo wa shule hiyo umeondoa adha hiyo kwa watoto wa kijiji hicho.
Aidha amesema kuwa, tayari Halmashauri, imeanza mchakato wa awali wa kusajili shule hiyo, na baada ya kukamilika wanafunzi, wataanza kupata Elimu shuleni hapo.
Hata hivyo wananchi wa Kiseriani tayari wameanza ujenzi wa maabara ya masomo ya sayansi ili kukidhi vigezo vya shule hiyo kisajiliwa.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.