.Na. Elinipa Lupembe.
Jumla ya Wanafunzi 7,018 waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka 2021 halmashauri ya Arusha tayari wameanza mosomo rasmi, katika shule sekondari za serikali walizopangia, kufuatia kufaulu mtihani wa darasa la saba uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2020.
Afisa Elimu sekondari, halmashauri ya Arusha, Mwl. Menard Lupenza, ameleza kuwa, jumla ya wanafunzi 7, 018 sawa na asilimi 88, waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kupangiwa kwenye shule za sekondari za serikali za halmashauri ya Arusha, tayari wameripoti shuleni na kuanza rasmi safari yao ya masomo ya elimu ya sekondari.
Afisa Elimu Lupenza amefafanua kuwa kati ya wanafunzi 7,886 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka wa masomo 2021, wanafunzi 7, 018 tayari wamekwisharipotii kwenye shule walizopangiwa na kuanza masomo yao ya sekondari ambapo kati ya hao 7,018 wasichana ni 3,153 na wavulana 2,746, na kuongeza kuwa kati ya hao, wanafunzi 607 wamehamia kwenye shule nyingine za serikali ndani na nje ya halmashauri ya Arusha.
"Kati ya wanafunzi 7,018, tumefuatilia na kugundua kuwa wanafunzi 512 wamekwenda kujiunga na shule za binafsi, na tumejiridhisha na uandikishwaji wa wanafunzi hao kwenye shule hizo za binafsi, lakini jumla ya wanafunzi 868, wasichana 432 na wavulana 436 sawa na asilimia 1, hawa bado hawajaripoti kwenye shule walizopangiwa, licha ya kuwa muda wa kujisajili unaendelea, jitihada za kuwatafuta wanafunzi hao zinaendelea kwa kushirikiana na maafisa watendaji wa kata na vijiiji na viongozi serikali za wa vijiji pamoja na wazazi na walezi wa watoto hao". Amefafanua Afisa Elimu huyo.
Naye mkuu wa shule ya sekondari Oldonyowas, mwalimu Richard Mugabuso amethibitisha kupokea jumla ya wanafunzi 67 kati ya wanafunzi 83 waliopangiwa, na kuongeza kuwa, jumla ya wanafunzi 63 walihamia shuleni hapo kutoka shule nyingine walizopangiwa na wanafunzi 12 wamehama kwenda shule nyingine za sekondari, huku wanafunzi 4 tu hawajaripoti shuleni hapo mpaka sasa.
Hata hivyo mkuu wa shule ya sekondari Mukulat, mwalimu Meiseyeki Saiboku, naye amethibitisha kupokea jumla ya wanafunzi 279 wavulana 117 na wasichana 163 kati ya wanafunzi 300, waliopangiwa shuleni hapo kuanza masomo ya sekondari Januari mwaka 2021.
Wakati huo huo, jitihada za ukamilishaji mradi wa ujenzi wa vyumba 52 vya madarasa, unaendelea vema lengo likiwa ni maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka ujao 2022, kati ya vymba hivyo 52, vyumba 42 viko hatua za ukamilishaji, vyumba 5 viko kwenye hatua ya lenta, vyumba 4 viko kwenye kupandisha kuta na chumba 1 kiko kwenye hatua ya msingi.
Awali uongozi wa halmashauri ya Arusha, unawataka wazazi na walezi ambao hawajawawezesha watoto wao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021, kuhakikisha wanafunzi hao wanarepoti kwenye shule walizopangiwa, na kushindwa kufanya hivyo, seriakli itawachukulia hatua za kisheria.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.